Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa,
zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali
itakayokua inazikabili.
Uzinduzi
huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la
Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho,
uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika
uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini,
jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo
ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi
wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na
kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.
Nianze
kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo
na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru
sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi
asubuhi hii katika shughuli hii.
Ndugu
mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa
shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama
hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua
kuenzi maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo
mambo matatu makubwa.
La
kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali
kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu
Tanzania.
Leo
hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa
makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi
wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa
TFF?
FAT,wakurugenzi
wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la
taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka
1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa
michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194.
No comments:
Post a Comment