ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 3, 2015

TAMASHA LA HISTORICAL MARATHONI KUFANYIKA BAGAMOYO JUNI 14 MWAKA HUU

 Msemaji wa kampuni ya Vision Investiment, Dominic Mosha katikati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na  tamasha la Historical Marathoni  katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Meneja mawasiliano wa kampuni ya Vision Investment Dorah Raymond na kulia ni Meneja wa Fedha wa kampuni ya  Vision Investment Fatma Mfundo.  

 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika  mkutano wa kutangazwa kwa Tamasha la Historical Marathoni litakalofanyika Bagamoyo wilayani Pwani.(Picha na Avila Kakingo)



Na Avila Kakingo.
WANANCHI  wameombwa kujitokeza kwa wingi katika kushiriki  tamasha la Bagamoyo historical Marathoni,litakaloanza kufanyika Juni 14 mwaka huu katika Wilaya Bagamoyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo,katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam,Msemaji wa kampuni ya Vision Investiment Dominic Mosha alisema kuwa Tamasha la mwaka huu  litakuwa na kauli mbiu ya  “ANZA KUKIMBIA, UJIKINGE NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA”, kauli hiyo ikiwa na lengo la kudumisha afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa kama Kisukari,shinikizo la damu Nk.kwa  mazoezi ya kukimbia mchakamchaka ambako kunapumguza matukio ya vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukizwa.

Amesema Washiriki katika tamasha hilo  wanatakiwa kujiandikisha kuanzia Juni 4 mwaka huu katika maeneo mbalimbali kama Quality Centre,Msasani Mall, Kibo Complex na Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Pia kwa washiriki katika tamasha hilo kwa washindi 200 wa mwanzo kwa half Marathoni watapata nishani, mshindi wa kwanza sh.laki tano, mshindi wa pili sh. Laki nne,mshindi wa tatu laki tatu,mshindi wan ne laki mbili, mshindi wa tano laki moja, na washiriki wa sita hadi wa kumi kuzawadiwa sh. Elfu hamsini.

No comments: