ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 13, 2015

ASKARI WANNE NA RAIA WATATU NDIO WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE UVAMIZI WA KITUO KIDOGO CHA POLISI STAKISHARI UKONGA.

Mkuu wa Jeshi la Poilisi nchini, Ernest Mangu akiongea na wanahabari mapema leo.

Askari wanne na raia watatu wamefariki Dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kituo kidogo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar kuvamiwa na watu wanaosadikika majambazi.

Majambazi hao waliokadiriwa kua wanane walivamia kituo hicho mida ya saa 4 usku Jumapili July 12, 2015 usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Enerst Mangu amesema lengo la majambazi hayo ilikua ni kuiba silaha zilizokuwepo kwenye kituo hicho kidogo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es salaam.

Akiongean na wanahabari IGP Ernest Mangu amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kusaidia kuwakamata majambazi hao na hatimae kufikishwa katika mkono wa sheria.

IGP Enerst Mangu aliwaambia wanahabari, Jeshi la Polisi litaongeza ulinzi katika vituo hivyo kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi wake.

No comments: