Mwanamuziki wa nyimbo za Ukombozi kwa Bara la Afrika, Mkongwe, Dorothy Masuka akiwa jukwaani katika shoo yake usiku wa Julai 19, katika tamasha la 18, la ZIFF 2015,Ngome Kongw upande wa Mambo Club. (Picha zote na Andrew Chale wa modewjiblog.com-Zanzibar)
Gwiji wa muziki Afrika, Bi Dorothy Masuka akiimba pamoja na Mtanzania, Sauda Simba wakati wa shoo hiyo..(Zanzibar) Mwanamuziki wa nyimbo za Ukombozi kwa Bara la Afrika, Mkongwe, Dorothy Masuka kutoka Afrika Kusini ambaye pia anatamba na wimbo wa ‘Hapo zamani’ usiku wa Julai 19 ameweza kukonga nyoyo za wadau wa burudani waliofurika katika tamasha la filamu za nchi za majahazi la 18, maalufu ZIFF, linaloendelea katika viunga vya Ngome Kongwe, visiwani hapa.
Katika shoo hiyo iliyoanza majira ya saa nne usiku, Bi. Dorothy Masuka alionyesha umahiri wake wa kumiliki jukwaa kwa kuimba nyimbo zake mbalimbali zilizotamba zamani na hadi sasa hali ambayo iliamsha shangwe kwa wadau wa burudani waliofurika ndani ya Ngome Kongwe upande wa Mambo Club.
Mbali na nyimbo hizo, pia aliimba wimbo wa Kunguni wimbo ambao ulipata kushangiliwa pia kwa shangwe. Hata hivyo katika shoo hiyo Bi Masuka alipata sapoti ya nguvu katika upande wa usindikizaji jukwaani kutoka kwa Mwanamama wa Kitanzania, Sauda Simba Kilumanga aliyeshika vilivyo katika uimbaji.
Miongoni mwa nyimbo hizo ni pamoja na HAPO ZAMANI, KUNGUNI na nyingine nyingi.
Awali gwiji huyo alikutana na waandishi wa habari kuelezea mambo mbalimbali ikiwemo suala la Mwafrika na kubainisha kuwakila mwafrika anabahati kuzaliwa Mwafrika hivyo kwa waafrika walio nje ya Afrika watambue kuwa ni wamoja licha ya kutofautiana kwa lugha, matendo na tabia lakini bado tutabakia kuwa chimbuko moja.
Gwiji huyo anasema ameweza kutembelea Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa zaidi ya mara sita huku akiwa mstari wa mbele katika juhudi za kupigania harakati za ukombozi wa mwafrika wakati wa ukoloni.
Pia ameweza kufanya shughuli za chama cha TANU wakati huo kabla ya baadae kuwa CCM, huku akiimba nyimbo za ukombozi sehemu mbalimbali ikiwemo ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania.
Biography:
Dorothy Masuka is a jazz singer who was born in Bulawayo, Southern Rhodesia in 1935, then called Southern Rhodesia. She was the fourth of seven children and her mother was Zulu while her father was a Zambian hotel chef.
Born: September 3, 1935 (age 79), Bulawayo, Zimbabwe
Albums: The Definitive Collection, Hamba Notsokolo and more. (By Wikipedia).




No comments:
Post a Comment