Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ACP David Misime
---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Nina
imani kila mmoja anayo taarifa kuwa wiki hii hapa Dodoma kutakuwa na Mkutano
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi. Mkutano huo utajumuisha Viongozi wa
Kitaifa na Wajumbe wengi. Kutokana na unyeti wa mkutano huo mawazo
na masikio ya watu wengi wa ndani na nje ya Tanzania watayaelekeza katika Mkoa
wetu kutaka kujua nini kinachoendelea.
Kwa vile
mkutano huo utakusanya watu wengi, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
likishirikiana na vyombo vingine vya Dola tumeimarisha ulinzi ili wageni na
wenyeji waweze kufanya shughuli zao kwa amani, usalama na
utulivu. Ulinzi huo umeimarishwa pamoja na mambo mengine ikiwa ni
pamoja na doria za miguu, magari, pikipiki na Mbwa na Farasi.
Ili Jeshi
la Polisi na vyombo vingine vya Dola waweze kufanya kazi hiyo kwa ufanisi,
linaomba ushirikiano wa Wananchi wa Dodoma na wageni kwa kutupa taarifa pale
watakapoona mtu/watu au jambo lolote linaloashiria uhalifu ili hatua za haraka
ziweze kuchukuliwa.
Aidha
wamiliki na wahudumu wa nyumba za kulala wageni waimarishe ulinzi wa maeneo
yao, kuwashauri na kuhifadhi mali za wateja na kutoa taarifa kwa Jeshi la
Polisi pale wanapoona watu/wageni wanaowahisi ni wahalifu, kwani uhalifu
ukitokea katika eneo lako ni dosari kwa biashara yako.
Pia
tunaomba kila mmoja atambue na kukumbuka kila mara kuwa ulinzi na usalama
unaanza na yeye mwenyewe kwanza.
Nitoe
onyo kwa wale wenye mawazo ya kupanga kufanya uhalifu wa aina yeyote ile uwe wa
kijinai au wa usalama barabarani atambue atashughulikiwa kwa nguvu zote kwa
mujibu wa sheria za Nchi na asitokee wa kumlaumu mtu kama atakuwa amevunja
sheria.
Niwashauri
wale wote ambao wanataka kuja Dodoma katika wiki hii kama hana shughuli maalum
inayomlazimu kuja ni vizuri asije ili kuepuka usumbufu maana wengine wanaweza
kuja tu kwa lengo la kuja kushuhudia kinachoendelea au kwa ajili ya ushabiki
tu.
Imetolewa
na
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma
No comments:
Post a Comment