ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 21, 2015

KANISA LA UMOJA DALLAS TEXAS - JULAI 19, 2015

Waumini wa Umoja Church Dallas TX  wakiwa katika picha ya pamoja Jumapili ya July 19, 2015 
Kanisa la Umoja Dallas, Texas Marekani linazidi kukua. Jumapili, Julai 19, mgeni rasmi aliyealikwa kutoka Tanzania Pastor Dr. Danel Moses Kulola alihubiri. Wengi walinufaika na mafundisho yake. Baada ya ibada Van mpya ya Kanisa hilo ilibarikiwa. Gari hili litatumika kuwasafirisha wale ambao hawana usafiri. Mkutano wa Usharika umeamua kuanzisha kanisa pale mjini Houston Texas mwishoni mwa mwezi wa Agosti 2015. Wengi wa washarika wa Umoja ni kutoka Tanzania, Kenya na Democratic Republic of Congo. Mchungaji Kiongozi ni Absalom Nasuwa kutoka Tanzania.
Pastors Sua, Kulola, Bocko & Chove wakiwa Umoja Church Dallas.
Watoto wakifurahia Van mpya ambayo itakuwa msaada mkubwa kwao

1 comment:

Anonymous said...

Mungu awahurumie kila njia mtajaribu.