Advertisements

Friday, July 3, 2015

KESI YA MRAMBA NA WENZAKE KUSIKILIZWA JUMATATU


Basili Mramba,Daniel Yona,Agrey Mgonja mwingine hakufahamika jina lake wakijadili jambo kabla ya kusomewa hukumu yao ambayo imeahirishwa mpaka tarehe 6 mwezi wa 7.

Daniel Yona, Agrey Mgonja wakisubiria hatima ya kesi yao inayowakabili katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar.

Ndugu na jamaa waliofika mahakamani hapo kusikiliza hukumu hiyo.

Mramba na wenzake wakijadili kabla ya hukumu yao ambayo imeahirishwa tena
Daniel Yona,Agrey Mgonja na Basil Mramba.

Kesi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamini Mkapa inayowakabili viongozi waliokuwa kwenye dhamana katika sekta mbalimbali akiwemo Waziri wa Fedha Basil Mramba,Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona, na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Agrey Mgonja imesogezwa mbele baada ya mwenyekiti wa jopo la Majaji John Utamwa kushindwa kufika Mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo kwa dhurula ya ugonjwa kwa ruksa ya daktari kwa siku mbili.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya mahakama, Hakimu Mkazi, Mheshimiwa Sauli Kilemela amesema kuwa kutokana na sababu za kiafya zinazomkabili mwenyekiti hawana budi ya kuahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 6 mwezi huu majira ya saa saba mchana kwa ajili ya kutoa hukumu.

Kesi hiyo inayowakabili akina Mramba inasemwa ni kwa sababu ya kulisamehe kulipa kodi Kampuni la Alex Stewart na kuisababishia serikali kupoteza kiasi cha shilingi bilioni 11.7

2 comments:

Anonymous said...

Kesi ya miaka 10 upuuzi mtupu

Anonymous said...

Vinara wa ufisadi. Ukifuatilia washitakiwa kwa makini utaona vitu fulani ambavyo washitakiwa wote watatu wanavyo.