Advertisements

Monday, July 27, 2015

Mbunge Edward Lowassa kakaribishwa UKAWA, amejiunga nao? Majibu ni haya kwa Mbatia… (Audio)


“Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje” Hii ni moja ya sentensi ambazo Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa aliziongea Arusha May 30 2015 alipotangaza nia ya Kugombea Urais kupitia CCM. SOURCE:MILLARDAYO.COM

4 comments:

Anonymous said...

Hii ni kichekesho cha mwaka!!!! Hivi huyu mbatia si ndiye yeye alimfitini mrema mpaka akaondoka nccr mageuzi, si hao hao chadema walimfitini zito na kumletea ubabe mpaka wakamvua uanachama. Si ndio hao hao cuf walifitini mzee bob makani mpaka akaondoka cuf. Sasa hawa wanajiita ukawa mbona hawaoni boriti ktk jicho lao!!! Wasanii wakubwa, kwanza ukawa sio chama cha siasa sasa wana agenda gani na ilani yao ni nini? Hao ukawa ndio walikuwa wanamwita lowasa fisadi papa sasa amekuwa msafi. Ikulu hauendi kwa sababu ni maarufu!!!! Unaenda kwa uchapakazi wako. Na ccm wana vigezo vyao vya kutomchagua lowasa. Na ukawa kama mnamtaka lowasa rudini kwanza kwa watanzania na mkanushe kauli zenu kwamba sio fisadi papa. Wote ukawa hamna ukweli wowote mlisema mgombea wenu mngemtangaza toka wiki mbili zilizopita lakini hadi leo hamjafanya hivyo!!! Mambo madogo kama kutangaza mgombea mnashindwa je maamuzi makubwa ya kuongoza nchi mtayaweza??? Vyama vyenu ubabe mwingi kila wakati wa uchaguzi wagombea wenu wa urais ni haoa hao ina maana hakuna demokrasia ya kweli na ubabe ndio umewajaa. Ikulu mtaendelea kuisikia tu wala hamtakaa mshinde mnatapatapa maana hamna sera yoyote zaidi ya kukosoa ccm. Tupe sera mbatia, vunjo tu ilikushinda sasa unatafuta umaarufu. Kwanza mapendepekezo ya katiba kutakuwa hakuna ubunge wa kuteuliwa uliopewa na rais Kikwete, acha unafiki kama kweli wewe ni mpenda mageuzi mbona hukukataa ubunge wa kuteuliwa na rais. Au ruzuku ndio kipaumbele kwako. Jamani msichukie ni kuelimishana tu na kuwekana sawa. Asante kaka luka kwa kupost comment yangu

Unknown said...

Hao ukawa wameishiwa kabisa nilidhani ni watu makini kumbe bure kabisa. Inaonesha dhahiri ukawa hawana mtu kabisa wa kumsimamisha kupambana na Mr. Bulldozer maghufuli mpaka wanakwenda kumuangukia mwaanausalama wa ccm mh lowasa. Lowasa na CCM sawasawa na king kibadeni na simba hawezi kuwa yanga hata kwa namna gani ile. Kikunge na lowasa na CCM lengo Lao kuidestroy ukawa na ukawa kwa kutaka kumkumbatia lowasa wanailifanya lengo la ccm kuwa rahisi kinyume na matarajio yao . Yaani ukawa kumlilia lowasa sawa na kutaka kuyakumbatia mauti. Kifo cha nccr mageuzi kilikuwa chini ya Augustine mrema hapana shaka ukawa kifo chao kipo chini ya lowasa kama wataendelea na matamanio yao ya kutaka kumsajili.

Anonymous said...

kwani hii picha inamwonyesha mheshimiwa amejiunga au inamwonyesha wakati anapewa rungu hilo kule nyumbani tena miaka ipatayo miwili. wanahabari mnaipotosha umma vibaya sana. hata haya maneno yamepangwa tu. Mwacheni Lowassa ale bata wake uzeeni..

Anonymous said...

Do The Math for CHADEMA:

If, LOWASA(ccm) + RICHMOND = UFISADI;
And, CHADEMA(Ukawa)) # UFISADI;
Then; CHADEMA + LOWASA = _?

NB: # represents "Not Equal To"