Advertisements

Monday, July 27, 2015

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA UKAWA NA WAHARIRI ULIOFANYIKA MAKAO MAKUU YA CUF

 Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba na wa pili kulia ni Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi.Katika mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.
 Mmoja wa waandishi mahiri kutoka gazeti la Raia Tanzania,Hafidhi Kidogo aikuliza swali kwa viongozi hao wa UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari na umoja huo,uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar.


Mkutano wa viongozi wa UKAWA na wahariri wa vyombo vya habari umemalizika na haya ndiyo yaliyoyazungumzwa;



Lipumba: Maswali ya ufisadi katika Tanzania ni maswala ya Mfumo, mfumo wa siasa ndio unaoendeleza ufisadi, Lowassa ameachia madaraka mwaka 2008, katika kipindi hiki ufisadi umeongezeka au yamepungua? Pia yeye mwenyewe alisema mwenye ushahidi aende mahakamani.



Swala la kumtangaza mgombea urais ni utaratibu wa vyama,Lakini nina uhakika Mwanzoni mwa mwezi August tutakuwa tumepata mgombea urais ambae atapeperusha bendera ya UKAWA.



Kuhusu Lowassa kupewa nafasi ya kugombea urais, Hilo ni swala la mchakato, mgombea urais atapatika kwa utaratibu ambao upo kikatiba.



Mzee Makaidi (NLD)

Lowassa ni mtu safi hadi pale atakapobainika mahakamani ni mchafu.



Mbatia: Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake. Watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi. Mwanzoni wa mwezi wa nane(wiki ijayo) tutamtangaza mgombea wetu kwa mbwembwe, tumeshapiga hatua ambayo ni nzuri. 



Mbowe: Mazungumzo yameshafanywa hivyo hawezi kuongea na amesema kuhusu picha za Lowassa kuwa kwenye kikao cha CHADEMA zimetengenezwa.



Lipumba: Kuhusu CUF kusuasua, UKAWA Chama chetu hakijasusua bali kilikuwa kinafuata taratibu za chama na mkutano mkuu umebariki, yeyote atakayechaguliwa kupitia UKAWA, mimi nitamuunga mkono, chama kimebariki maamuzi haya, unapozungumza na mwenyekiti wa CUF basi ndio unazungumza na CUF.

No comments: