ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 19, 2015

TASWIRA YA SHEREHE ZA EID MUBAKAH NEW YORK


Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhan Mwinyi Muombwa ndiyo alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo ya Eid Mubarah, hapa Mh.  akiongea mbele ya Watanzania kutoka sehemu mbalimbali kama New Jersey, Boston, Philadelphia, Connecticut na New York yenyewe.
Katika sherehe hizo watu walipata chakula cha jioni na watoto kupatiwa zawadi za michezo mbali mbali.

Mwenyekiti wa tawi la CCM New York Bwana Seif Akida akiongea machache.

Mwenyekiti wa NYTC Bwana Haji Khamis akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhan Mwinyi Muombwa


Layla Yahya wa Nawal Founder kutoka Swansea. UK nae alikuwapo kwenye sherehe hizo Nawal ni Project inayojulikana kwa jina la (Bigger Heart Zanzibar) maalum kwa kusaidia watoto wenye shida pale Zanzibar ukitaka kujua zaidi juu ya Project hii unaweza kubovya hapa na ujipakulie mwenyewe kiroho safi. http://www.biggerheart.org.uk/


Mmoja ya watoto walipata zawadi kwenye sherehe hizo akimuonyesha mama yake zawadi aliyopewa.


Baada ya mambo yote kwenda kama yalivyo pangwa ulifika muda wa kupata ukodak na mgeni rasmi kama unavyoona akina mama mbele ya camera ya vijimambo.


Akina baba nao wakipata ukodak na mgeni rasmi, kwa picha zaidi nenda soma zaidi.






3 comments:

Anonymous said...

mashallah mmependeza wenyewe wana new York.eid mubarrak wote huko. I hope mnapendana kikweli kweli hamna fitna fitna kama wenginewe.

picha huwa hazisemi uongo;ukiziangalia unaweza kujua hisia zenu.

nakutakiyeni mshikamano wa kweli wa kiislamu wenye kupendana kidhati na si kusengenyana.ameen.

Anonymous said...

Mashallah wenyewe, jicho la hasidi lisiwaone.

Anonymous said...

na lisiwaone na lisiwanoa amen ya rabbi laalamin.