ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 15, 2015

WAKILI ELIAS NAWERA ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM

Wakili Elias Nawera akionyesha alama ya dole baada ya kukabidhiwa fomu hizo. Kulia ni mgombea ubunge mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Lilian Mkosani.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kawe, kada wa chama hicho, Wakili Elias Nawera (katikati), Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni mgombea ubunge mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Lilian Mkosani
 Wakili Nawera (kulia), akiandika jambo kabla ya kulipa sh. 100,000  ya kuchukulia fomu.
 Hapa akimshukuru Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe baada ya kuchukua fomu hizo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimuelekeza Wakili Elias Nawera mambo ambayo anapaswa kuyafuata baada ya kukabidhiwa fomu hizo.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni ambaye anamaliza muda wake Iddi Azani akimpongeza Wakili Nawera baada ya kuchukua fomu hizo. Azan alifika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake ya ubunge katika Jimbo hilo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-)

3 comments:

Anonymous said...

Siasa imekuwa kazi yenye deal sana Tanzania. Ubunge si uwakilishi tena bali ni full professional. Hii yote ni sababu ni kazi inayolipa pesa nyingi bila kuumiza kichwa wala mwili. Naona kizazi kijacho chote kitakuwa cha wanasiasa. Hakuna anayefikiria uvumbuzi wa sayansi na teknolojia...ni siasa, siasa, siasaaaa tu TZ.

Mdau
Japan

Anonymous said...

Nakubaliana na mdau wa kwanza ,

Anonymous said...

Wee hapo juu umeongea kweli kabisa, inasikitisha.