Advertisements

Friday, July 3, 2015

WAUMINI WAANZA KULIOMBEA TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongea na Baadhi ya viongozi wa kidini wa Kikristo nchini.(picha kutoka maktaba)


Waumini wa madhehebu tofauti mkoani Tanga wameanza zoezi la kuliombea taifa katika mchakato wa uchaguzi mkuu ujao ili uweze kufanyika kwa amani na utulivu pamoja na kupata viongozi ambao watajali maslahi ya watanzania.
Wakizungumza katika ibada maalum ya kuliombea taifa pamoja na kuwasimika baadhi ya viongozi wa makanisa mbalimbali wamewataka watanzania kuacha kushabikia vyama na badala yake wachague viongozi ambao wataendelea kudumisha utaifa na kusimamia sera ambazo zitaleta maendeleo kwa taifa.
Aidha askofu wa kanisa la Free Pentekoste jimbo la Tanga mchungaji John Mwakyusa amewataka viongozi wa itikadi za vyama tofauti kutumia vyema majukwaa ya kisiasa katika kampeni zao kutoa lugha ambazo zitakuwa na elimu ndani yake kwa wananchi
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya viongozi wakuu wa madhehebu nchini wamewataka baadhi ya viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi mkuu kusimamia na kutekeleza ahadi zao ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi ambayo imesababisha maafa katika maeneo tofauti hapa nchini.

No comments: