Advertisements

Sunday, August 2, 2015

BABA NA MWANA WACHEZA MECHI TIMU TOFAUTI

Mchezaji wa Stars United Malik akipata picha na mwanae kabla ya mechi siku ya Jumamosi Aug 1, 2015 kati ya Stars United na All African Stars iliyochezewa Atlanta, Georgia. Katika mchezo huo Malik na mwanae walicheza timu tofauti wakati Baba akicheza kitasa mwanae akicheza nafasi ya ushambuliaji huku mtoto akisikika akisema anataka amwonyeshe baba mpira wa kisasa unavyochezwa na lazima ampite na kufunga bao, lakini katika mchezo huo baba alikua ukuta usiopitika kirahisi na kabla Malik kuumia katika dakika ya 67 ya mchezo Stars United walikuo mbele kwa bao 4-1 na baa da ya yeye kutoka ndipo All African Stars waliporudisha mabao yote na kupata lingine la kuongoza kabla ya Stars United kusawazisha dakika za majeruhi. Mtoto wa Malik kwa sasa yumo kwenye akademi ya watoto wanaotumainiwa siku za usoni kuchezea timu ya Taifa ya Marekani.

1 comment:

Anonymous said...

Very encouraging keep it Dad & Bab T.