Advertisements

Monday, August 3, 2015

F.O.D - rafiki wa maendeleo. FRIENDS OF DEVELOPMENTS

Kundi linaloundwa na wasanii wa filamu,wanamuziki na wanamichezo kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo yao na taifa kiujumla la Friends of Developments(F.O.D), limepania kufanya mengi makubwa kulisimamia jina lao la “Rafiki wa Maendeleo” kwa kufanya kazi za kijamii zikiwemo kusaidia wasiojiweza, kwa kujitolea na kufanya matamasha mbalimbali mfululizo na hasa kipindi hiki cha uchaguzi.
Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa FOD na pia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini IBRAHIM KAMWE “Bigright” amesema – FOD inayoongozwa na Rashid Nasor “chidy mzee wa mbele” recho na Crama tayari imeshajikusanyia wanachama zaidi ya milioni tatu wengi wakiwemo,wanafunzi wa vyuo, viongozi wa chama na serikali wazee kwa vijana.
Kwa kuwa FOD yenyewe ina simamia zaidi maendeleo , na kipindi hiki ni cha uchaguzi ikaweka muswada wa kumsapoti kiongozi wanayeona atawaletea maendeleo na ambaye tayari amekwisha fanya mengi yaliyoonekana ambaye ni John Pombe Magufuli.
FOD imedhamiria kwa dhati itajituma kila kona ya Tanzania kuhakikisha magufuli anakuwa madarakani washirikiane nae katika kulisukuma hilo gurudumu la kuleta maendeleo .

No comments: