Mpenzi wa hivi anaweza hata akawa anakulamba miguu mkiwa wawili tu ili ujue kuwa yeye ni wako. Lakini ‘taiming’ yake kubwa ni kufaidika.Wengine hufikia kukuganda kwa sababu umeshamuahidi mambo kibao. Umemuahidi utamjengea nyumba, utamsomesha, utamwendeleza kimaisha, utampangia chumba au kumnunulia gari, lazima atakupenda kwa sababu ya ahadi hizo tu na si vinginevyo.
MALENGO KIVIPI?
Kwanza naomba niwaanike watu wanaoingia kwenye mapenzi wakiwa na malengo yao. Hawa ni wale ambao wamekutana na mtu, wakasoma mazingira na kubaini kuwa, akiwa naye kiuhusiano, ataweza kupata vitu mbalimbali, kama pesa, kusomeshwa, kununuliwa nguo, kuendelezwa kimaisha na mambo mbalimbali yanayofanana na hayo.
MAPENZI YALIVYO
Mimi nasema mapenzi yanataka mchango. Mchango kwa maana gani? Kama kweli mnapendana, basi kila mmoja amuoneshe mwanzake kwamba ni kweli anampenda.Ziko njia nyingi zinazomfanya mtu ajue unampenda. Mawasiliano, kujuliana hali, kulindana na kufuatiliana. Hayo ni mambo yanayotakiwa kufanywa na watu wanaopendana. Na si yafanywe na mmoja tu anayempenda mwenzake.
BAHATI MBAYA ZILIZOPO
Lakini kwa utafiti wangu nimebaini kuwa, wako watu wawili kimapenzi lakini mmoja yupo kwa malengo yake na mwingine yupo kwa mapenzi ya dhati. Hawa watu wa hivi ni hatari sana. hatari zaidi kwa huyo mmoja mwenye malengo.Kama wewe unaishi au upo na mwenzako mwenye malengo lakini hana mapenzi ya dhati utamjua kwa haya ninayokwenda kuyasema hapa.
HANA WIVU NA WEWE
Upo na mwenzako kimapenzi. Lakini hata akikusikia unaongea na mtu mwingine kwenye simu tena mazungumzo yanayoashiria mapenzi, ukimaliza kuongea yeye hakuulizi huyo nani wala haoneshi amekerwa na mazungumzo yako. Huyo hakupendi! Ana malengo yake.
Upo na mtu kimapenzi, pengine anakuona umesimama na mtu ambaye si wa jinsia yako, mnaongea na mnacheka lakini yeye hatetemeki, wala moyo haumdundi! Huyo ana malengo yake. Ukiona hivyo, shtuka ndugu.
HAKUFUATILII
Mapenzi ya kweli lazima kufuatiliana kuwepo. Kama kweli huyo mpenzi wako anakupenda atapenda kujua ratiba zako zote. Atapenda kujua upo wapi na unafanya nini! Atapenda kujua unarudi nyumbani muda gani na kama hujarudi uko wapi na kwa nini upo huko?
Sasa utakuta unajigamba kwamba una mpenzi. Lakini mpenzi mwenyewe wala hakufuatilii kwa lolote. Ukivaa vizuri hasemi. Kama mnaishi mbalimbali, wala hakuulizi uko wapi hata giza likiingia. Unaweza kukaa mahali mpaka saa sita usiku lakini yeye wala hakuulizi uko wapi, unafanya nini wala kwa nini upo huko? Ukiona hivyo, huyo ana malengo yake.
MESEJI MPAKA UANZE WEWE
Mpenzi wa hivi naye ni tatizo! Unasema una mpenzi wako, anaishi wapi sijui! Lakini cha ajabu, hakutumii meseji ya kuhusiana na kitu chochote kile, mpaka uanze wewe.
Ukimtumia meseji ukamwambia, ‘I miss you’ eti na yeye ndiyo utamsikia.., ‘Miss you 2’. Ukipiga mahesabu utabaini kuwa, hata siku moja hajawahi kuanza kukutumia meseji yeye ya hata kukuuliza kama umekula!
Usiku ukiingia kama hamjaonana siku hiyo, yeye anadunda tu. Hata kukutakia usiku mwema hakupo. Saa mbili, saa tatu, saa nne, saa tano, mpaka unasinzia. Ikitokea ukaanza wewe, ‘usiku mwema’, ndiyo utamsikia na yeye, ‘na wewe mpenzi wangu jamani!’
AKILI ZA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO
Kila mtu ana akili zake timamu. Naamini wewe uliye ndani ya uhusiano, una akili zako timamu. Sasa kama ikitokea ‘ukabahatika’ kumpata mpenzi mwenye tabia hizi, akili za kuambiwa na mimi kwenye mada hii, changanya na zako utagundua kuwa, unaliwa, unaibiwa tu.
GPL
No comments:
Post a Comment