ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 14, 2015

JESHI LA POLISI NCHINI LAPIGA MARUFUKU MISAFARA YA KWENDA KUCHUKUA FOMU NEC PAMOJA NA KUSAKA WADHAMINI

          Na Lorietha Laurence –Maelezo. 


Jeshi la Polisi nchini limesitisha maandamano ya wafuasi wa vyama vya siasa wakati wa kuchukua ,kutafuta wadhamini, na kurejesha fomu za kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Inspekta Jenerali wa jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki amesema kuwa jeshi limechukua hatua hiyo kutokana na ukiaukwaji wa sheria za usalama barabarani uliojitokeza wakati wagombea wa vyama vya CHADEMA na CCM walipochukua fomu za kugombea Urais makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 

“Kwa sababu za kiusalama Jeshi la Polisi linasitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukua fomu, kutafuta wadhamini mikoani pamoja na zoezi la kurejesha fomu “ alisema Kaniki. 

Aidha aliongeza kuwa jeshi la Polisi nchini linafanya utaratibu wa kuwakutanisha wadau wote wa siasa ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi Mkuu ili kuona namna bora ya kufanya uchaguzi katika hali ya amani na utulivu. 

“Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua za kisheria mgombea, kiongozi, mfuasi au chama chochote cha siasa kitakachokiuka agizo hili,” alisema. 

Hatua hiyo ya jeshi la Polisi nchini inatokana na baadhi ya wagombea wa nafasi za Urais kufuatana na kundi kubwa la wanachama, na wapambe wao wakati wa kuchukua fomu za kuomba kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi hivi karibuni na kuhatarisha usalama ikiwemo kufungwa kwa barabara na kusababisha baadhi ya shughuli za kijamii kusimama.

4 comments:

Anonymous said...

Hawa jeshi la polisi nao wasitufanye sote wapumbavu kwa kutaka kumfurahisha bwana wao CCM hizi kupiga marufuku zisizo kwisha kwa sababu hali ni mbaya kwa sasa kwa upande wao, sherehe na ngoma zinaruhusiwa kama ccm wana uhakika na ushindi lakini kwa kasoro zilizo jitokeza kwa sasa za UKAWA tujitayarishe kwa hizi marufuku za kila siku.

Huu ndio mfumo wa vyama vingi jeshi la polisi hawana elimu ya kutosha kuhusu mfumo huu na kama wanayo basi maafande wao upande wa chama cha mapinduzi wanawasukuma kama walevi kwa amri za kipuuzi,fanyeni kazi kwa utaratibu wa kulinda AMANI sio woga wa kupiga marufuku kila kitu mchezo huu umekuwa chaka la kuto kufanya kazi zenu ndio maana mnapata matatizo mengi bila kujua uvivu/tatizo liko wapi imani ikiwa toka wananchi na jeshi hili hamtoweza kuwazuwia kufanya wanacho taka nafikiri hili mlizingatie mapema kabla hatari huu ni ushauri tu.

Anonymous said...

wewe anonymous wa 8:12am kweli shule yako ndogo sana. kwa hiyo wewe unaona wanavyofanya ccm na chadema kukusanya makundi makubwa na kuzuia shughuli za kiuchumi kuendelea ni sahihi kwako. watu wanashindwa kufanya kazi, biashara kwa sababu ccm na chadema wanakusanya watu barabarani badala ya viwanja vya mikutano. kwa hili polisi wako sahihi kabisa na watanzania wote tuunge mkono jitihada zao za kulinda usalama. acha ushabiki wa kisiasa katika suala la usalama wa nchi. nenda shule ujue jinsi ya kufafanua mambo sio tuu unakuja hapa katika blogu ya wananchi unaanza kutoa mapovu.

Anonymous said...

Wewe Anomy wa 10.50
Nafikiri u kibaraka wa CCM usiyetaka maendeleo kW Watanzania
Kulinda usalama kwa wapinzani
Huyo Magufuli anapita Kila kona kujinadi
Na barabara mnafungua wakati mkijuwa Fika yeye ni waziri wa ujenzi na mgombea urais
Mmeanza kampeni kabla ya wakati wewe babu Lubuva huyaoni haya
Magufuli alikota mwanza hadi dar watu wangapi walichelewa kazini, shuleni toka mwanza hadi dar
Mtajuta mwaka huu

Anonymous said...

Wewe Anomy wa 10.50 am: nyamaza kimya! Jeshi la polisi linatumiwa kwa kazi ambazo haziko katika sheria zao za kazi. Wanapaswa tu kuarifiwa kwamba kuna mkutano au maandamano. Kazi yao ni MOJA kuhakikisha kuna amani PERIOD!