ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 9, 2015

LOWASSA AHUDHULIA MKUTANO WA BARAZA KUU LA CHAMA CHA WANANCHI CUF JIJINI DAR LEO

 Sehemu ya Wafuasi na Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF, wakiwa wamejipanga Barabarani tayari kwa kumlaki, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akielekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungua Wanachama na Wafuasi wa Vyama UKAWA waliofurika kwenye Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akikumbatiana na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kabla ya kuelekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakiwapungia wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. Wengine walioambatana nao ni Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi.
 Wanachama wa Chama cha Wananchi CUF wakifurahia Ugeni huo.
 Sehemu ya Viongozi wakuu wanaounda UKAWA, wakiongozwa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi, Mh. James Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi, wakimsuburia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi wakitembelea kuelekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakiwapungia wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. Wengine walioambatana nao ni Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi.

Umati wa Watu ukiwapokea Viongozi wao.
Umati nje ya Makao Makuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasili kwenye Makao Mkuu ya CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi,Mh. James Mbatia  akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwahutumbia maelfu ya wanachama na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, nje ya jengo la Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kabla ya kufanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akimpongeza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa mara baada ya kuhutubia.
Wakielekea kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Mh. Magdalena Sakaya wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho, uliofanyika August 9, 2015, kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.

5 comments:

Anonymous said...

Kwa kumpokea Fisadi Lowasa na baadhi ya waliokuwa makada wenzake wa CCM, sina shaka kusema kwamba UKAWA wamepoteza kete muhimu sana, ambayo ilijengeka katika dhamira ya kupiga vita ufisadi na ya kupigania katiba inayokidhi matakwa ya wananchi wote wa Tanzania.

Sasa ni wazi kwamba UKAWA wanataka kuiondoa CCM madarakani for a wrong reason: kwamba sasa ni zamu ya UKAWA kushika dola ili nao wanufaike na ufisadi! That's what I am now hearing! They simply cannot have it both ways: kwamba wawe na mgombea kinara wa ufisadi, ambaye pia alishiriki kukataa Katiba ya Tume ya Warioba, na wakati huo huo waweze kupiga vita ufisadi na kutetea Katiba ya wananchi (iliyopendekezwa na Tume ya Warioba).

Nilikuwa nimewekeza kisaikolojia kwenye upinzani kwa muda mrefu kwa kudhani kwamba wapinzani watatuletea mabadiliko ya kweli, lakini sasa wamenifungua macho UKAWA wenyewe kwamba kumbe zile kelele zao za kila siku sio kelele za kutetea maslahi ya wananchi wote wa Tanzania, bali ni kwa ajili ya kupigania fursa na maslahi yao wenyewe. Sawa, now I know; UKAWA tuongee baada ya mimi kupunguza hasira zangu October 25!

Anonymous said...

Anonymous wa kwanza inaonekana wewe ni ccm na inakuuma sana,pole sana ndugu yangu ndio siasa ilivyo ni mchezo mchafu,na hao makada wa ccm wanaomfuata lowasa mbona bado subiri aanze campaign nadhani ndiyo utakufa kwa kihoro itabidi utafute ndimu na mbili mbili ndugu yangu,tatizo lenu mlizoea sana utawala dume wa ccm na mungu kawaona watanzania kwa nyie kumkata lowasa,na lowasa anakubalika na kwa taarifa yako wanaomkubali ni wananchi ambao hawako chama chochote ata kabla hajahama ccm,ukiunganisha na nguvu ya UKAWA ccm lazima wakae.

Anonymous said...

Its funny pale mtu ambae unaona kabisa ni mwana ccm alafu anajifanya UKAWA,mtoa maoni wa kwanza ni mwana ccm ila anazuga sababu inamuuma kwa edo kwenda UKAWA,kama ukweli umechoka na ccm ulikuwa ufarahie kuvurugika kwa ccm ili watu wengine waje na wapimwe utendaji kazi na kama hawawezi wataondelewa waje wengine ili wajue kwamba unapopewa madaraka usijisahau kwamba utakuwa pale forever,mtu mwenye akili timamu utaiteteaje ccm?kwa lipi unless hujatembea vijijini kujionea huduma za jamii zilivyodumaa sababu ya utawala dume wa ccm,mambo yote wanadai waliofanya ni misaada ya wazungu especially barabara anazojivunia kikwete,its time for changes na uzuri watanzania wameaamka,na hawadanganyiki kwa propaganda Kama za wewe anonymous wa kwanza ,people they already set their mind,wameshasoma alama za nyakati.

Anonymous said...

mwalimu alisema mpinzani wa kweli wa ccm atattoka ndani ya ccm. pia aliwahi sema watu wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya ccm basi watatafuta nje ya ccm. vipi wewe anonymous wa kwanza ni mtafuta mabadiliko au ni miongoni mwa wale ambao hawahitaji mabadiliko. AMKA NA ANZA KUWAZA JUU YA MABADILIKO KWA AJIRI YA KIZAZI CHA LEO NA KESHO.

Anonymous said...

Sasa ni wakati wa kutoa jembe na kuweka trekta na kutoa nyondo na kuweka nail gun mabadiliko muhimu tumechoka na ccm bado inafuata mifumo ya kale anayebisha angalie alama zake bado ni jembe na nyundo nani katika karne hii anataka kutumia zana hizo