ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 10, 2015

MBOWE NA KAMANDA KOVA WATOLEA UFAFANUZI KUHUSU MAANADAMANO YA KUMSINDIKIZA MGOMBEA URAIS KUCHUKUA FOMU

 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema kuwa UKAWA hawana taarifa zozote za zuio la maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu Mgombea wao wa Urais Mh. Edward Lowassa yanayoanzia ofisi za CUF hadi tume ya Uchaguzi (NEC).
Kwa upande wa Jeshi la Polisi ,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, amesema kuwa maandamano wanayo yatambua ni yale yanayoanzia CHADEMA kwenda NEC na kurudi Chadema makao makuu kinondoni, lakini ya kutoka makao makuu ya CUF buguruni kwenda NEC hawayatambui.

 Jeshi la Polisi jijini Dar limeafiki maandamano ya kumsindikiza kuchukua fomu mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa kwenda NEC kuanzia ofisi za CUF.

4 comments:

Anonymous said...

polisi sasa watakuwa wapuuzi wanataka kuzua vurugu watu wafe na waumie halafu watasema wapinzani sioni sababu yoyote kuzuia watu kumsindikiza kipenzi wao hata kama watatoke CUF kwanza kama wanamsindikiza kwa Amani silioni tatizo hapo.

Anonymous said...

Hata polisi wanna hofu na ukawa ninawashauri wasome nakuona nyakati ktk nchi nchi yet.

Unknown said...

hawa polisi wa ccm ni majanga, mbona magufuli alidindikizwa na kulikua hamna neno?? ukawa ikichukua nchi hivi ndo vyombo vinavyotakiwa kusafishwa haraka!!

Anonymous said...

Hayaaaaaa, hayawi hayawi ndio hayooooo. Raisi wetu.....tuna imani na Lowassa