OFISI ya Makamu wa Rais inasikitika kuwepo kwa taarifa ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyotambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais.
2 comments:
Kusema ukweli JK aliwatema huyu na MP kama vile wasingeweza kumridhi mikoba hao ni watendaji wakuu wa nchi mimi nilijua kama miaka ya nyuma ktk 5 bora hizo nafasi mbili zilikuwa zimejazwa hivyo watafute watatu Zaidi lakini walitemwa lazima watakuwa na ya moyoni lakini wananyamaza kwa sasa hawataki lawama lichama litakapondondoka kama embe mbovu mpiga kura independent.
Lipo, lipo, kama halipo linakuja
Post a Comment