ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 16, 2015

MKUU WA JESHI MSTAAFU WA BURUNDI AUAWA

Chief Colonel Jean Bikomagu, enzi za uhai wake.

Mkuu wa Jeshi Mstaafu wa Burundi aliyongoza mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, Chief Colonel Jean Bikomagu ameuawa kwa kushambuliwa na risasi nyumbani kwake leo na watu wasiojulikana.
Mmoja wa wanafamilia alikiambia chombo kimoja cha habari mjini Bujumbura kuwa, Jean Bikomagu alivamiwa na watu wasiojulikana mapema leo nyumbani kwake Wilaya ya Kinindo, Kusini mwa Mji Mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura, akiwa kwenye gari na binti yake. Baada ya kuvamiwa, wauaji hao walimmiminia risasi nyingi hadi kumuua na kumjeruhi binti yake kasha kukimbia na pikipiki kusikojulikana.
Haya ni mauaji ya pili mfurulizo kwa makamanda ngazi za juu wa Jeshi nchini Burundi tangu wiki mbili ziishe sasa. Agosti 2, Jenerali, Adolphe Nshimirimana aliyekuwa karibu na rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza kuvamiwa na kuuawa nyumbani Mjini Bujumbura.
Jenerali Adolphe Nshimirimana, enzi za uhai wake.

Jeshi la polisi na mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa, gari alimokuwa Nshimirimana lilishambuliwa na rocketi na kumiminiwa risasi nyingi siku ya Jumapili asubuhi hadi kusababisha kifo chake.

No comments: