Mwanariadha Mo Farah amefanikiwa
kutwaa taji lake la dunia na kwa kutetea taji lake la mbio za mita
10,000, licha ya kupoteza balansi katika raundi ya mwisho na kutwaa
medali ya kwanza ya dhahabu kwa Uingereza katika mbio za Mabingwa
Duniani.
Mo Farah akichuana na wakenya Kamoror na Tanui
Miaka saba iliyopita katika uwanja huo huo wa Jijin Beijing nchini China, Farah aliaondolewa katika michuano ya Olimpiki baada kushindwa kufuzu mbio za mita 5,000.
Hata hivyo katika mbio za mwaka huu, Farah alionyesha kujituma ili kuhakikisha anawashinda wapinzani wake kutoka Kenya Geoffrey Kamworor na Paul Tanui.
Mo Farah akisujudu kumshukuru Mungu kwa ushini
No comments:
Post a Comment