Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto Mhe.Dkt Pindi Chana (Mb) akiangalia baadhi ya machapisho yanayohusiana mbinu za malezi na makuzi ya watoto kabla ya kufungua semina ya siku mbili ya matokeo ya utafiti wa malezi na makuzi ya familia nchini iliyofanyika Hotel Protea Courtyard, jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto (Mhe. Dkt Pindi Chana (Mb) akifungua rasmi Kongamano la siku mbili la wadau wa familia wanaokutana kupokea matokeo ya utafiti wa malezi na makuzi ya watoto katika familia lililofanyika hotel Protea jijini Dar es salaam, tarehe 26/8/2015.
Kulia; Naibu Waziri Mhe.Dkt Pindi Chana (Mb)akisikiliza maelezo ya utangulizi ya Kongamano la Utafiti wa Malezi na Makuzi ya Watoto katika Familia (kushoto) ni Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bibi Nuru Millao aliyeongozana na Mhe. Naibu Waziri katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la familia katika hotel ya Protea, jijini Dar es salaam tarehe 26/8/2015
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Utafiti wa Malezi na Makuzi ya Watoto katika Familia wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Mhe. Dkt. Pindi Chana (MB hayupo pichani) katika Hotel ya Protea Courty yard jijini Dar es salaam tarehe 26/08/2015.
No comments:
Post a Comment