ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 26, 2015

WENGI WAMSINDIKIZA KUCHUKUA FOMU MGOMBEA UBUNGE WA CCM, MBARALI.

Mgombea Ubunge PirMohamed akiwasili wilayani Mbarali kwa ndege binafsi alipoondea kuchukua fomu.
Maandamano ya magari na pikipiki yakimsindikiza kuchukua fomu mgombea ubunge wa CCM
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Matayo Mwangomo akimkabidhi barua ya kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo hilo PirMohamed kabla ya kuelekea kuchukua fomu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Adam Mgoyi akimkabidhi fomu ya kuwania kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM PirMohamed.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi(CCM) Jimbo la Mbarali, Haroon PirMohamed akivalishwa skafu na Green guard baada 
yakuwasili katika ofisi za Chama hicho.
Mgombea Ubunge PirMohamed akiwa mepokelewa na Halmashauri kuu yaCCM Wilaya ya Mbarali.
Mgombea ubunge akiwa kwenye msafara wa kuelekea ofisi ya Mkurugenzi kuchukua fomu.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mbarali, Abdalah Mpokwa akizungumza katika mkutano wa kumtambulisha mgombea ubunge.
Wanachama wa CCM na wananchi wakiwa wamefurika katika mkutano wa kumtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Mbarali.
Mgombea ubunge Jimbo la Mbarali, Haroon PirMohamed akizungumza na wananchi wa Mbarali katika mkutano wa kujitambulisha.

MGOMBEAUbunge wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Mbarali Mkoania Mbeya HarounPirimohamed Mulla amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM katika ofisi ya mkurugenzi wa uchaguziwilayani humo kwa kusindikizwa na umati mkubwa wa wanachama na wananchi wenye niana upendo na chama hicho.

Wananchi haoambao wengi wao ni wapenzi wa chama cha mapinduzi CCM,walijitokeza juzi asubuhikatika uwanja wa ndege mdogo uliopokatika shamba la Mbarali Estates na kumlakimgombea huyo kwa shangwe mara baada ya kushuka ndani ya ndege binafsi na kishakuanza msafara wa
kuelekea katika ofisi za CCM wilaya na baadaye katika ofisi za mkurugenzi wa uchaguzi.

Mgombea huyoalisindikizwa na magari zaidi ya 50 na pikipiki zaidi ya 70 na mara baada ya kuchukua fomu ya kuwaniaubunge,aliwahutubia wananchi mbalimbali waliofurika katika viwanja vya ofisi yachama cha CCM wilayani Mbarali na kuahidi kuwa akishapata ridhaa ya kupitishwakatika uchaguzi ujao atahakikisha anawatumikia wananchi.

Alisema mudawa maneno matupu umepitwa na wakati na kuwa katika kauli mbiu yake ya ‘’Manenokidogo kazi zaidi’’ ina maana kubwa sana ya kuhakikisha kuwa anawaleteamaendeleo wananchi katika maeneo tofauti ya jimbo hilo na kuwa uwezo wakuwatumikia anao.

Mgombea huyoHaroun Mulla alisema mikakati yake ni kuwaletea maendeleo ya pamoja wananchi wajimbo hilo wakiwempo akina mama,wazee na Vijana na kuwa atahakikisha anaachahistoria ya kasi ya maendeleo il iwe mfano kwa wabunge wengine watakao kujasiku zijazo. Akizungumza kwakujiamini,Mulla alisema muda wa maneno matupu umekwisha na kuwa watanzaniawanataka kazi na vitendo zaidi na kubainisha kuwa kama mgombea wa CCManaukakika wa kufanya hivyo ndani ya muda mfupi mara baada ya kuchaguliwa nawananchi wa jimbo la Mbarali.

Kwa upandewake,Mwenyekiti wa chama cha CCM Wilaya ya Mbarali,Mathayo Mwangomo alisemachama cha CCM kimempata mgombea ambaye anakubarika,anauzika na ambaye ni mtu wavitendo kutokana na kuchangia shughuri za maendeleo kabla ya kugombeanafasi yaUbunge katika jimbo hilo.

‘AkiwaMwanachama wa kawaida ndani ya CCM amekuwa mshirika mkubwa katika kuchangiashughuri
za maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo nakuwa ushindi wake ndani yaCCM unatokana na misingi aliyojiwekea na wananchiwengi wa jimbo hili wanamuunga mkono’’alisema Mwangomo.

No comments: