Advertisements

Wednesday, August 26, 2015

Magufuli akataa Mawaziri.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake ya awamu ya tano haitakuwa na blablabla katika utendaji wa kazi na kuonya kuwa waziri atakayeshindwa kutelekeza majukumu yake, ataondolewa ili kupisha wenye uwezo.

Dk. Magufuli alitoa ahadi hiyo jana, wakati akijinadi kwa wananchi wilayani Nkasi na Kalambo, mkoani Rukwa akiwa katika siku ya pili ili achaguliwe kuwa rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Alisema Baraza lake la Mawaziri ni lazima liwe na tofauti kubwa kwani watakuwa watumishi wa watu na siyo mabosi wa watu.

Alisema waziri atakayeteuliwa katika serikali hiyo, atampima na akiona hawezi kutumiza majukumu yake ipasayo kwa wananchi, lazima aondolewe na nafasi yake ichukuliwe na waziri mwingine mwenye kasi ya kufanya kazi kama yake, vinginevyo atawafukuza kila mara.

Dk. Magufuli ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi, alisema atafanya hivyo kwa sababu wananchi wanataka matatizo yao yatatuliwe kwa wakati na si kusubiri siku inayofuata.

“Baraza langu litakuwa la kutetea wanyonge, litafanya kazi za wananchi, nachukia uzembe na nitaonyesha kwa vitendo,” alisema na kuongeza kuwa serikali yake itahakikisha fedha zinapelekwa kwa wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Ifike mahali tunaadhimisha wiki ya maji na maji yapo, wiki ya nyama na nyama zipo, wiki ya Ukimwi na dawa zipo na wiki ya maziwa na maziwa yapo,” alisisitiza. Vilevile, aliwaonya watendaji wazembe akisema hawana nafasi kwani mwendo wake utakuwa ni wa mchakamchaka na hakutakuwa na mapumziko hadi maendeleo yawafikie wananchi. Mgombea huyo aliahidi kuunda serikali isiyo na kero kwa wananchi wa ngazi zote, wakiwamo wa kipato cha chini, na itakuwa mkombozi kwa mamalishe na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kuwa itahakikisha zinafikia mwisho.

NEEMA KWA MADAKTARI
Kwa upande mwingine, Dk. Magufuli aliahidi kuboresha mishahara na maslahi mengine kwa madaktari na wauguzi ili kudhibiti wizi wa dawa za serikali na kuziuza kwa wagonjwa kwenye maduka yao na kusababisha hospitali, vituo vya afya na zahanati kukosa dawa.

“Tunataka hospitali na zahanati zetu ziwe na dawa za kutosha, mwananchi apate huduma nzuri,” alisema.
Kadhalika, alisema serikali yake ina mpango wa kujenga zahanati katika vijiji vyote, vituo vya afya kwenye kata, hospitali wilayani na hospitali za rufaa mikoani ili kusogeza huduma za matibabu karibu na wananchi na kuwaondolea kero ya kusafiri kufuata huduma hiyo mbali na makazi yao.

ELIMU BURE
Dk. Magufuli aliahidi kuwa akiingia madarakani baada ya kuchaguliwa, kitaumbele cha kwanza kitakuwa ni kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne huku akiwataka Watanzania kuzaliana kwa wingi kwa kuwa serikali itabeba jukumu la kusomesha watoto wao.

Alisema fedha za kutekeleza hilo zipo kwa kuwa atakuwa amedhibiti mafisadi na wezi wa mali za umma.Mgombeaurais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake ya awamu ya tano haitakuwa na blablabla katika utendaji wa kazi na kuonya kuwa waziri atakayeshindwa kutelekeza majukumu yake, ataondolewa ili kupisha wenye uwezo.

Dk. Magufuli alitoa ahadi hiyo jana, wakati akijinadi kwa wananchi wilayani Nkasi na Kalambo, mkoani Rukwa akiwa katika siku ya pili ili achaguliwe kuwa rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Alisema Baraza lake la Mawaziri ni lazima liwe na tofauti kubwa kwani watakuwa watumishi wa watu na siyo mabosi wa watu.

Alisema waziri atakayeteuliwa katika serikali hiyo, atampima na akiona hawezi kutumiza majukumu yake ipasayo kwa wananchi, lazima aondolewe na nafasi yake ichukuliwe na waziri mwingine mwenye kasi ya kufanya kazi kama yake, vinginevyo atawafukuza kila mara.

Dk. Magufuli ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi, alisema atafanya hivyo kwa sababu wananchi wanataka matatizo yao yatatuliwe kwa wakati na si kusubiri siku inayofuata.

“Baraza langu litakuwa la kutetea wanyonge, litafanya kazi za wananchi, nachukia uzembe na nitaonyesha kwa vitendo,” alisema na kuongeza kuwa serikali yake itahakikisha fedha zinapelekwa kwa wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo.

“Ifike mahali tunaadhimisha wiki ya maji na maji yapo, wiki ya nyama na nyama zipo, wiki ya Ukimwi na dawa zipo na wiki ya maziwa na maziwa yapo,” alisisitiza. Vilevile, aliwaonya watendaji wazembe akisema hawana nafasi kwani mwendo wake utakuwa ni wa mchakamchaka na hakutakuwa na mapumziko hadi maendeleo yawafikie wananchi. Mgombea huyo aliahidi kuunda serikali isiyo na kero kwa wananchi wa ngazi zote, wakiwamo wa kipato cha chini, na itakuwa mkombozi kwa mamalishe na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kuwa itahakikisha zinafikia mwisho.

NEEMA KWA MADAKTARI
Kwa upande mwingine, Dk. Magufuli aliahidi kuboresha mishahara na maslahi mengine kwa madaktari na wauguzi ili kudhibiti wizi wa dawa za serikali na kuziuza kwa wagonjwa kwenye maduka yao na kusababisha hospitali, vituo vya afya na zahanati kukosa dawa.

“Tunataka hospitali na zahanati zetu ziwe na dawa za kutosha, mwananchi apate huduma nzuri,” alisema.
Kadhalika, alisema serikali yake ina mpango wa kujenga zahanati katika vijiji vyote, vituo vya afya kwenye kata, hospitali wilayani na hospitali za rufaa mikoani ili kusogeza huduma za matibabu karibu na wananchi na kuwaondolea kero ya kusafiri kufuata huduma hiyo mbali na makazi yao.

ELIMU BURE
Dk. Magufuli aliahidi kuwa akiingia madarakani baada ya kuchaguliwa, kitaumbele cha kwanza kitakuwa ni kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne huku akiwataka Watanzania kuzaliana kwa wingi kwa kuwa serikali itabeba jukumu la kusomesha watoto wao.

Alisema fedha za kutekeleza hilo zipo kwa kuwa atakuwa amedhibiti mafisadi na wezi wa mali za umma.
CHANZO: NIPASHE

4 comments:

Anonymous said...

Jamani hizi nyimbo ni zile zile na weingine kupromiss kuleta meli Dodoma.....why wait mpaka uwe raisi na siku zote hamkuweza .....kweli siasa ni SI HA SA....i am sure watu wanakubali uongo huu bado.

Anonymous said...

Kama ni ukweli wanataka elimu itolewe bure kwanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha
Nne siwangefanya hivyo miaka yote hamsini na zaidi wakiwa madarakani ni nini kilichowazuia au niuongo mwingine wa kutaka kuendelea kuwaibia na kuwakandamiza Watanzania

Anonymous said...

Ndio siasa ni Si HA SA Ukawa juzi tu madomo Yao yalikuwa mapana kuliko ya kiboko yakiwaeleza watanzania jinsi lowasa anavyonuka ufisadi eti leo hii ananukia uadilifu tangu lini ? tena watu walivyokuwa hawana hata haya na uongozi wa chama wamempa huo ni ulofa wa hali ya juu.

Anonymous said...

Jinsi hii kero za waTanzania itakuwa ndotonkuisha na ESCROWS zitaendelea hadi kilio. Kila waendako utasikia ilani ya chama, tutatekeleza madawa yawepo hospitalini?!! Hahaahh hizi ni ndoto za kusadikika! Mkipewa leo.kwsho matatizo yameanza mtatumaliza jamani. Kero hamziwezi mkiwa ndani ya ilani ya CCM ya kulindana
A hogue machifu basi
Nasikia kisha ajira kwa waliokosa kura za maoni
Kaani mkao wa kula
Sasa makapi tukaneni Ukawa , na Lowassa kwani ajira mmnazo kwa matusi yenu
Hongera ilani ya CCM