ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 29, 2015

FFU-UGHAIBUNI WANAZO SABABU ZOTE ZA KUMKUBALI JOHN MAGUFULI

Kiongozi wa bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya
Ngoma Africa band, Kamanda Ras Makunja amefunguka kwa kusema kuwa
yeye na kikosi kazi chake wanazo sababu zote za kumkubali mgombea urais wa chama tawala Mheshimiwa John Pombe Magufuli ashinde kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi mkuu utakao fanyika 25 oktoba 2015.Mkuu huyo wa Ngoma Africa band akikaririwa bila kigugumizi ameweka wazi kuwa John Magufuli anatufaa kuwa Rais wa nchi yetu na tunazo sababu zote za kumkubali,mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja amewaomba watanzania wote bila kujali itikadi na ushabiki wa vyama vyao wapigie kura za NDIO John Pombe Magufuli na Bi.Samia Suluhu Hassan. Mwanamuziki huyo aliweka wazi kuwa Tanzania tunahitaji
Rais mchapa kazi,Mkweli,mwenye umri ambao sio kijana mno wala sio mzee,rais mwenye maadili,kueshimu sheria na katiba ya nchi ,tunahitaji Rais anayeyajua machungu na kero za watanzania pia awe ameshapitia maisha ya kawaida ya mtanzania ,si mwingine bali John Pombe Magufuli

9 comments:

Anonymous said...

Ignorant man!

Anonymous said...

Ni vema kama tunatafuta watunishaji misuli Tanzania tumkubali Magufuli, Lakini kama tunataka mabadiliko ni vema tuwe wakweli kwamba CCM hawana sera mpya. Nijambo la fedhea sana mgombea urais badala ya kusimama jukwani na kutoa sera kwa wananchi anaanza kuwachezea wananchi kwa kupiga push up. Mwananchi ameacha shughuli zake kuja kukusikiliza ili apate ujumbe unaoweza kumpa matumaini. Badala yake unaanguka chini unaanza kupiga push up, huo ni utoto. Naomba waheshimiwa muhache kujidhalilisha wenyewe. Push up zibaki kwa vijana wa mitaani na walevi wakipimana nguvu.

Anonymous said...

bhangi ni kitu kibaya sana kwa afya ya akili.

mdau
texas

Anonymous said...

Rasta wa FFU unaishi ughaibuni hujui hata chembe matatizo tunayopata ndugu zako nchini chini ya utawala wa ccm. Tafadhali ni bora kukaa kimya kuliko kuongelea vitu ambavyo huna experience navyo.

Anonymous said...

Ccm mbovu ila Magufuli Jembeeee hana mpinzani,,

Anonymous said...

kama push up ndiyo sera basi tumeishiwa....tutabaki beba box na ujinga

Anonymous said...

Punguza jazba. Kwani ni sera zipi unazipata kwa kumsikiliza Lowasa kwa dakika 3 ?

Anonymous said...

Need to think outside the box.kwa CCM to Ukawa message sent kuwa hatuwezi kuruhusu wagonjwa waongoze nchi.He fooled the Ukawa lakini hawezi kuwa fool watanzania wwote . Ni rahisi kuweka Gym ikulu kuliko kufungua ICU.

Anonymous said...

Hakuna ubaya "push up" na sera zikienda sambamba. Magufuli anawaonyesha wananchi kuwa ana afya nzuri na yuko tayari kukabiliana na mikiki mikiki ya ofisi ya urais. Pamoja na haya yote baada ya "push ups" zake amekuwa anamwaga sera za chama chake na hivyo kukidhi matakwa ya wananchi wanaotaka kujua sera hizo na hivyo Kutowapotezea muda wao. Ndiyo maana wananchi wengi wamekuwa wanamshangilia na wengine kuanza hata kuigiza sathili yake hii wakijua kuwa afya ni bora kwa kila mtu ili kuweza kukabiliana na msatakabali wa maisha. Hii ni tofauti na mgombea wenu ambaye hawezi hata kusimama wala kuwahutubia wananchi kwa muda wa maana, sana sana dakika 5 - 10. Tofauti nyingine na mgombea wa CCM ni kuwa mgombea wenu wa Ukawa kwa kutokuwa na sera ya chama chake anachofanya ni kulalamika tu na kutoa ahadi za uongo na anazojua hawezi kuzitekeleza hususan kwa muda anaotaja. Kwa mantiki hii CCM itaendelea kukoga mioyo ya Watanzania kwa muda mrefu ujao.