Katika hali ya kushangaza na kusikitisha tarehe 6/09/2015 siku ya Jumapili mjini Tabora mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema Ndg. Edward Lowassa aliamua kutumia udini kuomba kura.
Ndg. Lowassa akihudhuria ibada katika kanisa la Kilutheri (KKKT) mjini Tabora amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii akidai kuwa, kwa kuwa toka nchi ipate uhuru hajawahi kutokea Rais kutoka dhehebu la Kilutheri hivyo mwaka huu ni zamu ya Walutheri.
Chama Cha Mapinduzi kinalaani matumizi ya lugha zinazoligawa Taifa letu kwa misingi ya udini, ukanda, ukabila na ubaguzi wa aina yeyote kisa tu kutafuta madaraka.
Kauli hii ya Ndg. Lowassa licha ya kuwa ni kinyume na Sheria za Uchaguzi za nchi yetu, kinyume na Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zilizosainiwa na vyama vyote, lakini ni kinyume kabisa na mila na desturi za Kitanzania katika kuhakikisha Taifa hili linabaki kuwa Taifa moja lenye umoja, amani na mshikamano.
Kwa mfano, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015, yaliyotolewa na Tangazo la Serikali Na. 294 la tarehe 27/7/2015 chini ya kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, ukurasa wa 5 kifungu 2.1(k) kinasema:-
“Viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao wahakikishe kuwa majengo wanayotumia kufanya kampeni sio ya Ibada. Vile vile, vyama vya siasa vihakikishe kuwa havitumii viongozi wa dini kupiga kampeni kwa ajili ya vyama vya siasa au wagombea wao”.
Lakini katika maadili hayo hayo, ukurasa wa 7, kifungu 2.2(i) kinasema:-
“Vyama vya siasa au Wagombea hawaruhusiwi kuomba kupigiwa kura
kwa misingi ya UDINI, UKABILA, JINSIA AU RANGI.”
Kwa kuwa Ndg. Lowassa siku hizi tabia ya kusahau inaongezeka kwa kasi nimeona ninukuu vifungu hivi kwa rejea yake na wenye tabia kama yake.
Lakini matamshi hayo ni uthibitisho tosha kuwa Ndg. Lowassa, Chama chake cha CHADEMA na vyama vinavyomuunga mkono chini ya UKAWA ni wabaguzi, wachochezi na waroho wa madaraka wasiojali masilahi mapana ya nchi yetu. Kwao madaraka ni muhimu kuliko nchi yetu.
Hii si mara ya kwanza kwa Ndg. Lowassa, Chama chake cha CHADEMA na makada wenzake kutoa kauli na kufanya vitendo vya kibaguzi, kwa kutumia ukanda na sasa wameamua kutumia udini kama njia ya mkato ya kutafuta madaraka.
Chama Cha Mapinduzi kinaamini huu si msimamo wala utamaduni wa Watanzania, bali ni uroho binafsi wa madaraka wa Ndg. Lowassa na chama chake, hasa baada ya kuona kuwa hoja zake za kutafuta nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi yetu zimekataliwa na wananchi.
Mwalimu aliwahi kutuonya juu ya wanasiasa wanaotumia udini na ukabila kama hoja ya kutaka kupata madaraka kuwa ni wanasiasa walifilisika kisiasa lakini ni watu wa hatari sana kwa mustakabali wa amani, umoja na mshikamano wa nchi yetu.
Hivyo basi, Chama Cha Mapinduzi kinalaani kauli hii na tunaamini inapaswa kulaaniwa na wote wanaoipenda nchi yetu. Lakini CCM inaamini vyombo vinavyohusika na hasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itachukua hatua zinazostahili kuondoa mbegu hii ya kansa inayoletwa na Ndg. Lowassa kwenye nchi yetu. Maneno ya Ndg. Lowassa ni kansa mbaya kwa nchi yetu na lazima yakemewe na kukomeshwa kabisa.
Maneno na vitendo vya Ndg. Lowassa, chama chake, na makada wenzake wa CHADEMA na vyama shirika vya UKAWA toka wameanza kampeni katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kwa nyakati tofauti zimejaa ghiriba na ubaguzi uliokithiri. Tabia hizi za Ndg. Lowassa ni moja ya sababu iliyopelekea CCM kutompa nafasi ya kugombea kupitia Chama hichi.
CCM inatoa wito kwa wadau wote na Watanzania wote kuwa ni vizuri kuwa makini wakati huu wa Uchaguzi, kuhakikisha hakuna jambo linaligawa Taifa letu. Tuendeshe kampeni bila kuligawa na kuliangamiza Taifa letu. Tanzania yetu ni muhimu. Tanzania kwanza mengine baadae.
Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
08/09/2015
12 comments:
Acheni porojo msituvuruge sidhani kama hata ingekuwa kuomba kura msikitini ingekuwa shida. Lazima kieleweke mwaka huu ccm pumzikeni.
Nape, ukiwa na jipya andika barua nyingine.
Ukisikia kuishia na sera/hoja au kufilisika kisiasa ndo huko sasa. nape wewe tunakujua kwa kuropoka ropoka ovyo. hatukushangai. tafuta jipya uandike. kwa taarifa yako CCM kimenuka. una jipya, hatuambiliki LOWASA RAIS WETU WA AWAMU YA TANA, penda usipende.
ukawa mbele kwa mbele.
NAPE UWE MKWELI MBELE ZA MUNGU WARAKA HUU SI WAKO NI WA YULE YULE ANAYEKUTUMA SIKU ZOTE.MAELEZO YAMEJAA PUMBA NA SHOMBO,YAMEJAA LONGOLONGO,KWA LOWASSA KILA MNAPOMSEMA CHART YAKE YA USHINDI INAPANA.JANA SEPTEMBA 9,2015 KABLA HUJAWEKA HUU UZANDIKI WAKO USHINDI WA MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA ULIKUWA UNASOMEKA KWA ASILIMIA 78.LEO HII SEPTEMBA 9,2015 USHINDI WA MHESHIMIWA LOWASSA BAADA YA KUFYATUKA KWAKO NAPE NI ASILIMIA 80.WEE LETA TUU ZAKO AZIDI KUPAA
Nape mwaka huu lazima povu likutoke ukizinagatia kule Mtama umeshapigwa chini kabla ya october 25, jipange kaka, chunga mdomo wako ukijua kuna maisha baada ya uchaguzi mkuu.
Mkuki kwa nguruwe
Babu kipara alvyotuita malofa , wapumbavu na kagera kasema sisi in mbumbu
Lubuva hakuyaona ya jangwani
Kayaona ya Kanisani
Hata mtoto aliyekwenye mimba hadanganyiki kiasi hiki
Uhuru wa uchagzi ni kwamba kila mgombea kura ana uhuru wa kufuata wafuazi wake popote pale walipo: kanisani , msikinini,barabarani na popote pale anapopata nafasi ya kuuza sera yake ili wafuasi wake wampe kura. Kama Kiongozi wa Kanisa au Msikiti anahutubia kumpendelea kiongozi fulani, hapo anavija sheria na utaratibu wa uchaguzi. Lowassa au Magufuli wanaweza kwenda popote pale wanavyotaka kwa sababu wanaomba kura. Wananweza kupata au wasipate hiyo ndio riski yao. Lowassa ametumia stategy ya kwenda Kanisani- matakeo yake atanvuna au asivune october 25, 2015
Pamoja na maelezo yako,inabidi utambue kila jambo lina taratibu zake.kuomba kura based on gender, religion, tribe, etc ni kukiuka taratibu za NEC.
Kabisa mheshimiwa Nape umeongea point ya maana. Watu waliokuwa wa pumba ndio watakaobeza kauli yako lakini watanzania makini tunalaani kitendo hicho cha lowasa cha kutumia udini katika kampeni zake . Huyo mzee anajijua hana muda atajifilia mbali kwa hivyo kwa hisia zake yeye hana cha kopteza hata kama nchi itaingia katika machafuko. Huyo lowasa ni mgombea wa aina gani anechochea ukanda, ukabila, udini pamoja na sifa yake kubwa ya ufisadi huyo ni mgombea wa aina gani? mafala pekee ndio yatayokuwa yanamuunga mkono.
Boko boko hili
Mchicha mwiba mdomo juu Kama kunguru weusi
Mwanaume mzima ovyo
CCM nashindwa kuelewa Kati ya wanaume na wanawake bora nafasi hizi wapeni wanawake wakisema na kubwatuka tutawaelewa
Lakini kuwapa wanaume Kama nape na kinanana toba mnawadhalilidhsha. CCM
Mpeni cheo hiki Kopa shangingi la mipasho
Tupashane hapa
Hujui usemalo au hukusoma na kuyaelewa malalamiko dhidi ya Lowasa. Tatizo sio kuomba kura kutoka kwa waumini bali ni madai kwamba nchi haijawahi kuwa na Rais muumini wa Lutheran, akimaanisha kwamba sasa ni zamu yake yeye muumini wa Lutheran. Man, it doesn't even take a high school diploma to understand this!
Nonsense; fanatics like you always write about nothing!
Post a Comment