
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumapili Sept. 20.15. Kushoto ni Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Charles William Iteba. PICHA ZOTE/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG

Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akizungumza wakati akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia) na Mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo, Charles William Iteba katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
![]() |
| Kippi Warioba akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano huo. |

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akipongezwa na wanaCCM baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
![]() |
| Kippi Warioba akibadilishana mawazo na Mmoja wa makada wa CCM waliohudhuria mkutano huo. Kulia ni Mkewe Nkaleni Warioba. |
![]() |
| Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Zarina Madabida akiongozana na Kippi baada ya mkutano kumalizika. |
Mtoto
akiwa bango lenye picha ya Kippi Warioba.
Na
Mwandishi Wetu
MGOMBEA
ubunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba,
amesema anafahamu changamoto zinazowakabili wamachinga, mamalishe, baba lishe
na wajaririamali wadogo; na kuomba wamchague ili azishughulikie.
Aidha,
baba mzazi wa mgombea huyo, Jaji Joseph Warioba, amewataka wakazi wa Kawe
wamchague kijana wake kwa kuwa ni msikivu, anayejituma na siyo mtu wa
kusukumwa.
Akizungumza
kwenye mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Songas ulipo Kata ya Makongo Juu
juzi, Kippi alisema amewahi kufanyakazi na sekta binafsi ambayo ilimkutanisha
na wajasiriamali, vikundi vya ujenzi, Saccos na Vicoba, hivyo alifanikiwa kujua
changamoto zinazowakabili.
“Changamoto
za makundi haya nazifahamu, nafahamu mnahitaji mafunzo na rasilimali mbalimbali
kuendesha biashara zenu nithibitisheni Oktoba 25 nikazifanyie kazi,” alisema.
Kuhusu
Makongo Juu, Kippi alisema Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, imeainisha kwamba
barabara ya Makongo kuanzia Chuo cha Ardhi hadi Goba itajengwa kwa kiwango cha
lami na tatizo la maji litakwisha kwa kuwa serikali itakamilisha mradi wa kutoa
maji Kimbiji hadi Dar es Salaam.
Matatizo
ya michango mingi shuleni ambayo wazazi wanailalamikia, uhaba wa madawati,
matundu ya vyoo, vitabu na madawati ni mambo ambayo tutashirikiana kwa pamoja
kuyatatua wala hayahitaji mipango mikubwa ya serikali,” alisema.
Alisema
wakazi wa Kawe wanapaswa kumchagua Dk. John Magufuli, yeye (Kippi) pamoja na
madiwani wa CCM ili wakamsaidie kazi ya kutekeleza ilani.
Naye
Jaji Warioba alisema wakazi wa Kawe hawapaswi kufanya makosa ya kuchagua
wagombea wa upinzani kwa kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi wa Magufuli,
itafanyakazi nzuri.
Alisema
Dk. Magufuli ni mtendaji mzuri asiyependa rushwa hivyo ni wajibu wa wananchi
kumchagulia wasaidizi kutoka CCM ili wakafanyekazi ya kuwatumikia.
Alisema
hulka za Dk. Magufuli zinafanana na za mtoto wake (Kippi), kwa kuwa naye ni
mchapakazi, msikivu na mtu mwenye ushirikiano mkubwa.
Naye
mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo Juu, William Iteba, alisema kero za wakazi
wa kata hiyo zinajulikana ikiwamo ukosefu wa kituo cha polisi, soko na ajira;
hivyo







8 comments:
Unapotuambia barabara itajengwa kwa kiwango cha lami??!! Hivi ni leo imeanza kuwepo au imejengwa? Ndani ya ilani hiyo unayosema nakuambiabmiaka mitano ijayo utaniambia!!? Labda ufisadi ndani ya chama ufe kwanza. Nani amfunge paka kengele?? Sio ndani ya chama wala uongozi!?!?
mzee warioba tangu usemwe ukiwa na jersey za ccm kwa mara ya kwanza tangu uonekane nazo hapo 1995, sasa umeamua kwa mara nyingine uzikunje uweke sandukuni,sawa.uelewe kitu kimoja ukawa haitokua na huruma kwa usaliti wako uliouonyesha wa kuikataa katiba mpya uliyoisimamia na kuitetea,iliyo sababisha makonda akuvurumshie magumi pale mlimani city.wewe kwa sasa ni msaliti wa daraja lile lile la dr.slaa,profesa lipumba,christopher mtikila,zitto kabwe na wengine unaowajua wewe[kwa sababu mnawasiliana]`mwisho wa ubaya aibu,jiandae kusutwa mara baada ya mheshimiwa lowassa kuapishwa.
Mh. Warioba Sinde tulikuamini sana lakini umewatosaa WaTanzania kapuni, bado unaona CCM Inaweza kuendelea kuwaletea maendeleao ndani ya katiba waliyochakachua ile uliyopokea ya wanannchi na ukaikubali walipoichakachua ulilalamika na bado inashangaza unaendelea kuwa nao, kama kweli unapenda waTanzania waendelee kufaidi matunda ya nchi yao na ukiwa kiongozi uliyekomaa, hebu mara moja achana na kusimama majukwaa ya CCM na urudi upande wa pili ili ulete mabadiliko usiwe mwoga umeshatumikia TAIFA hili na huhitaji Uraisi wala uMakamu!! Mze wetu Kingunge alisema ukweli na amekaa kimya ila nawe mzee tunakuomba urejee upande huu ili tutengeneze taifa huru lenye amani na kutokomeza umimi.. asante.
Kuapishwa wapi wakati Ikulu sio mahali pake?
Watu wa jembe na nyundo wana roho ngumu? Yani hawakubali neno sahihi lipite bila ya kuongeza pumba zao. Jamaa wamemkanda Warioba clearly for his bigotry but hawaoni hizo facts wanapinga tu mamvi kuapishwa. Hivi siku akiapishwa ni kweli watajiua ama? Mimi nachojua any thing is possible under the sun.
Mambo mengine sio lazima kubisha. Let it go sometime
BANANA REPUBLIC
TATIZO LA JAJI MSTAAFU WARIOBA NI BUNDA LA PESA HARAMU ZA CCM ALIZOKABIDHIWA KUPITIA KWA HUYU MWANAE KIPI MGOMBEA UBUNGE CCM-KAWE.JINGINE NI KUENDEKEZA NJAA,KILEVI,TAMAA,MATATIZO YA MFUMO WA FAHAMU.UNAJUA HAKUNA DHAMBI CHAFU YA AIBU KAMA USALITI.MSALITI BAADA YA KUFICHULIWA,SIKU ZOTE MAISHA YAKE HUGEUKA,NA HII NI AMRI YA MUNGU,KUGEUKA HUKO HUANDAMANA NA MSONGO MKUBWA WA MAWAZO,HALLUCINATIONS,GOING OUT OF NUTS NA HATIMAYE PERMANENT BRAIN TUMOUR.NYINYI WAFUATILIENI HUYU SINDE WARIOBA, DR.SLAA,PROFESA LIPUMBA,CHRISTOPHER MTIKILA NA ZITTO KABWE MTAKUJA TUAMBIA.
Ni kweli mambo mengine siyo vizuri kubisha lakini ukweli hapa pamoja na kuwa kitu chochote kinaweza kutokea lakini manvi haingii hawezi kuapishwa kwani hana hizo sifa na hakuna mtu atayejiua kwa ajili hii.
Post a Comment