ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2015

CHADEMA WATAMKUMBUKA DK SLAA MARA BAADA YA UCHAGUZI


Jana katika mahojiano na Tiddo Muhando kwenye kipindi cha Funguka, Zitto Kabwe amewaonya wana CHADEMA wanaomtusi Dr Slaa kwa sababu ya Lowassa kuwa watamkumbuka baada ya uchaguzi. Watu makini kama Dr Slaa na Prof Lipumba
wanaondoka na watu eti wanamuona Lowassa leo kawa bora?
Zitto kasema hivi sasa CHADEMA msingi wake umekuwa ni "Lowassa" na si kupambana na ufisadi tena. Baada ya uchaguzi hakutakuwa na CHADEMA ile tuliyoifahamu na ndipo hapo watanzania watakapomkumbuka Dr Slaa.

8 comments:

Anonymous said...

kweli huyu ameongea kweli kwani hapo nyuma walimsema kwa ufisadi nakumchafua lkn sasa hivi ndio wanajifanya wapo naye ,mimi naona hapo ni unafiki tu unatawala na ina maana bila Lowasa chama chao hakiwezi kitu na kisingekuwa na mgombea.

Atley Kuni said...

Zitto umenena, ushabiki mandazi ni kitu hatari sana nachelea kusema wakati tunajiandaa na uchaguzi mkuu wa 2015. ajenda kuu kote nchini ilikuwa ni Vita dhidi ya ufisadi na chama chochote ambacho kingesimamisha mtu anaye tajwa kwenye ifisadi basi chama hicho kingetoswa. Nawshukuru CCM walitii wakamuacha Lowassa. Lakini kwa masikitiko makubwa CDM wakamchukua na kumkumbatia. Na lakushangaza hata ule Wimbo wa Mafisadi siki hizi CDM hawaupigi kwa maaana wanajua walicho kifanya kuwa sio sawa.

Anonymous said...

Acheni ushabiki maandazi. Siasa ni propaganda. Haingii akilini fisadi asifikishwe mahakama mda wote ule. Kama ni kweli ni fisadi basi hatuna serikali ila kuna kundi la wanjanja likiongozwa na CCM

Anonymous said...

Zitto ni mmojawapo wa mafisadi pia kwa kukubali kutenda jazi kwa unafiki. Hakuna jipya analoliteta zaidi ya kuendelea kupokea hongontoka Chama tawala!!

Anonymous said...

Sio kweli!! nasema sio kweli wewe zito kujiona mtabiri mbona umetoka cdm hata hamna aliyekukumbuka zaidi ya kuitwa yuda? acha unafiki zito. Nyerere alisema ukila nyama ya mtu hutaacha kuila daima popote uendako. ulipokua chadema ulitaka kupindua uongozi kwa naraka za siri wewe na kitilya. umeenda act na sasa umesema juzi juzi tu utagombea urais mwaka 2020 ile hamu ya nyama ya mtu inaendelea.kwa nini. kwa sababu unataka kumpindua mgombea uraisi wa act hata kabla ya kuisha miaka yake kumi kwa dhana ya kuwa akichaguliwa kuwa raisi 25/10/2015 wa act ina maana atakaa kwa vipindi viwili 2015 hadi 2025 lakini wewe unataka umpindue 2020 si unaona ile zambi bado inakufuata?
acha unafiki kama umeishiwa sera stay shut up

Anonymous said...

Mnafiki mkubwa kazi yake kupayuka ovyo tu. Hana jipya!! Nani atabadilishwa na maneno ya kipumbavu. Mfuate Dr Slaa alikoenda unafiki hatutaki. Lowassa ni mpaka Ikulu hatubadiliki.

Anonymous said...

Slaa ni mnafki kama huyu Zitto kama kweli alimwona Lowassa fisadi inakuaje na kukiri kuwa yeye ndio mtu wa kwanza kutoa wazo la kumleta Lowassa CDMA ? Lowassa kahamia CDMA anaona uraisi ataukosa anaanza kuleta majungu. Richmond tushajua ukweli haikuwa Lowassa peke yake na hata ripoti ya Mwakyembe imesema wazi kuna majina hawawezi kuyatoa "usalama wa nchi" Ni kina nani hao majina yao yakitolewa yatahatarisha usalama wa nchi ?

Anonymous said...

Mwenye kupenda kweli hata akiona chongo huita kengeza. Nyinyi endeleeni kumshabikia tu huyo chongo wenu lakini Zitto, Dr. Slaa na wengine wameshawaeleza ukweli. Chama mmekiua kwa kumwingiza huyo fisadi.