ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 14, 2015

KIJANA FRANK ANAMTAFUTA BABA YAKE

Kijana FRANK MASANJA anamtafuta baba yake mzazi aitwae MASANJA BASU . Masanja alikuwa anaishi kwa kaka yake aitwae SHINGERA BASU sehemu iitwayo NYAKATO SOKONI mkoani MWANZA. Kabila la Masanja ni msukuma wa mkoani Shinyanga wilaya ya Bariadi katiki kijiji kiitwacho BUDARABUJIGA na jina la ukoo wao ni BASU. 
Sasa hivi wilaya ya Bariadi ipo ndani ya mkoa mpya waSimiyu na si Shinyanga tena. Mke wa kaka yake alikuwa mwalimu wa shule ya msingi. Baadhi ya watoto wa kaka yake ni BUSARU na MAEGA.
Masanja na kaka yake awali walikuwa wakiishi Shinyanga na kuamia Mwanza na kuwa wanafanya biashara ya madini wakiyafuata Nyarugusu, Singida Manyoni, Geita na sehemu zingine nyingi. 
Masanja alikutana na mama wa mtoto huyo aitwae SIWEMA ZABRON aliyekuwa akiishi kwa shangazi yake aitwae mama Jumanne sehemu iitwayo MEKO hapohapo mkoani Mwanza na mwaka 1995 Frank akazaliwa.
Frank alikwenda kumtafuta baba yake mwaka jana (2014) huko nyakato sokoni na kukuta nyumba waliokuwa wakiishi baba yake imeuzwa na kuambiwa kuwa wameamia Dodoma. Frank kwa sasa anaishi jijini Dar es salaam na mama yake.
Kwa yoyote anayemfahamu au kumfahamu mtu yeyote aliyetajwa hapo juu au kumjua mtu aliyekaribu na ukoo huo anaombwa kumsaidia kijana huyo aweze kumpata baba yake.
Asanteni na Mungu awabariki.
Mawasiliano
Namba za simu za mama Frank
+255 654 092813 au +255 755 451213
Namba za whatsapp za Frank +255 716627814

No comments: