Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Joseph Nyamhanga alisema hayo katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam. Alisema uzinduzi huo wa barabara ya Kidahwe – Uvinza utafanyika katika kijiji cha Kidahwe wilaya ya Kigoma na Daraja la Kikwete katika mto Malagarasi una urefu wa mita 275 na barabara unganishi.
“Ujenzi wa barabara hii ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kurahisisha usafirishaji katika mkoa wa Kigoma. Barabara hii imegharimiwa na serikali ya Tanzania pamoja na serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kupitia mfuko wa maendeleo wa Abu Dhabi kwa gharama ya Sh bilioni 82.044,” alisema.
Nyamhanga alisema ujenzi wa daraja hilo na barabara unganishi umegharimiwa na serikali pamoja na serikali ya Korea kupitia Benki ya Exim ya Korea kwa gharama ya Sh bilioni 90.974.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment