Pichani kati ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde kwa pamoja wakiwapungia wananchi wa jimbo la Mtera (hawapo pichani),ndani ya mji wa Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakazi wa jimbo la Mtera huku akiwamwagia sera zake za kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais katika awamu ya kipindi cha tano,mapema jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibakwe,Wilayani Mpwapwa,Ndugu Dkt.Simba Chawene akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa kijiji cha Chipogolo (hawapo pichani),wakati akitokea Iringa vijijini akielekea mkoani Dodoma kuanza kampeni zake mkoani humo,kulia kwake ni Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwatazama wananchi waliokuwa wakimuuunga mkono kuwa watampa kura za ndio
Dkt Magufuli akiwapungia Wananchi wa kijiji cha Chipogolo Wilayani Mpwapwa,mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Alhaji Adam Kimbisa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Kada mkongwe wa chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.John Samuel Malecela akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni.
Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli
wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli
Wanannchi wakifuatilia mkutano wa Dkt Magufuli katika kijiji cha Pawaga na Idodi mapema leo asubuhi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni akimalizia kiporo cha baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa aliyoanza kampeni zake hapo juzi mkoani humo,ambapo leo amewasili mkoani Dodoma na kuanza kampeni zake wilayani Mpwapwa katika jimbo la Kibakwe na baadae jimbo la Mtela.
4 comments:
Hata kwenda kumzika waziri mwenzio
Una roho ya paka magufuli
Kwani ungewaachia wengine wakupigie kampeni ungekosa nini
Hii inadhihilisha watanzania tukiwa na shida Kama una Safari ya USA utakwenda utuwache
Watanzania angalieni rais gani huyu
Hata Kama ratiba imepangwa
Jee Kama baba yako angefariki usinge kwenda kwenye mazishi kisa urais
CCM kifo cha Mende Huna washauri Kama jk
katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 CCM imeonyesha utovu mkubwa sana wa nidhamu kwa mambo,viashiria na ustaarabu wa kawaida wa watu wazima.la kwanza kubwa,na tena hili ni kubwa kabisa ni matumizi ya nguvu kubwa sana,kupindukia ya pesa.pesa hizi zimekuwa zikitumika visivyo kwa kuzigawa kama RUSHWA kwa kuwanunua wananchi ili wawaunge mkono,kuwanunua viongozi legelege wa vyama vya upinzani ili wavisaliti vyama vyao,kuwanunua wasanii mbali mbali kwa bei mbaya kabisa na kuwapatia nyenzo mbali-mbali vikiwemo magari ya bure,pikipiki,baiskeli,huduma ya posho kubwa sana kila siku-kwa sababu wamekuwa ni sehemu ya msafara wa mgombea urais wa ccm mhe.john magufuli na mgombea mwenza samia suluhu.kwa suala hili la rushwa CCM NI NAMBARI ONE KWELI-KWELI.PILI ni suala zima la kampeni chafu,za hovyo,za matusi makubwa na mazito dhidi ya mgombea urais wa chadema[ukawa] MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA na pia viongozi wengine woote wa UKAWA.Hili imekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa kawaida wanachama wa ccm,wale wasio na vyama,na pia wanachama wa ukawa ambao nao kama raia wengine wanajitokeza kwa wingi kuwasikiliza CCM wanasemaje kuhusu sera zao na jee yapo matumaini mapya ya kuyainua maisha duni ya watanzania wa leo?tunaishia kusikiliza MVUA YA MATUSI MLENGWA MKUBWA AKIWA MHESHIMIWA LOWASSA.Hakuna[litteraly] kiongozi yeyote wa ccm ambaye amepanda jukwaa mwaka huu AKAACHA KUMSHAMBULIA MHESHIMIWA LOWASSA,HAKUNA,ANZIA MKAPA,KIKWETE,MANGULA,KINANA,MSEKWA,MALECELA na wengineo wote- wote.KWA MFUMO HUU WA CHUKI INAYOENDELEA KUPIKWA NA CCM,MIMI NAAPA NA KUWAHAKIKISHIA CCM KUWA WAMEMPANDISHA SANA CHART YAKE MHESHIMIWA LOWASSA WANANCHI WANAJENGEWA HASIRA KUBWA NA CCM NA WATAISHUSHA KWA VITENDO HASIRA HIYO MNAMO JUMAPILI TAREHE 25 OCTOBA 2015 kwenye masanduku ya kura.MHESHIMIWA LOWASSA ATASHINDA KWA KURA NYINGI MNO ZISIZO NA UTATA WALA SINTOFAHAMU.HILI LITAKUWA FUNDISHO LA MAISHA KWA CCM NA HUSUSANI VIONGOZI WAKE. NGl
Hivi wala rushwa na wanaotoa hela kununua na kughiribu akili za wapiga kura ili wawaunge mkono ni nani kama siyo Ukawa? Hivi waliokuwa wanatoa hela kwa wana bodaboda kununulia petroli ili waungane na mgombea kwenye kampeni zake ni nani kama siyo Ukawa? Hawa wanaoandika matusi katika blog hii ni nani kama siyo wapenzi wa Ukawa? Hao wanaovamia misafara ya kampeni za CCM na kuingilia kati wakati mgombea wake akiongea ni nani kama siyo Ukawa? Hao wanaovurumsha mawe na chupa kwa polisi ni nani kama siyo Ukawa? Hawa waliomwaga mkojo kwenye ofisi ya CCM ni nani kama siyo Ukawa? Kuna kosa gani CCM kumsema Lowassa kama fisadi wakati nyinyi wenyewe mlimshambulia hivyo hivyo alivyokuwa CCM? Sasa hilo mnasema ni matusi, ama kweli "mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu uchungu"!!! Ukawa mnatakiwa kuwa wastaarabu. Kuwa na vyama tofauti au kuwa na mawazo tofauti kusiwe chanzo cha ugomvi kati yetu. Sisi wote ni Watanzania hivyo tunatakiwa tuendeleze utamaduni wa mshikamano na umoja wetu kwani baada ya uchaguzi kutakuwa na rais mmoja tu ambaye sote tunakiwa tumuunge mkono na kumkubali ili alitumikie taifa letu kwa lengo moja tu la kutuletaa maendeleo.
Nyinyi ukawa mtabakia makelele tu kama mliochananyikiwa. Nyinyi.ndio mlioyaanza haya yote mlifikiri CCM itakaa kimya bila ya kukujibuni. Mlizunguka nchi nzima mkiwaambia watanzania kuwa lowasa ni fisadi sasa leo kwanini CCM isiwakumbushe watanzania mliochokuwa mkikisema? Kwani hapo mlipokuwa mnangataza vita zidi CCM mlikuwa hamjui kama CCM ni miongoni mwa ya taasisi yenye nguvu barani Africa kama sio ya kwanza.sasa kwanini tena mnalia lia kama Ali yanga?
Post a Comment