ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 29, 2015

WAFUASI 60 WA CHADEMA AKIWEMO MGOMBEA UBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA MATATANI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA MAWE MKUU WA FFU NA WANANCHI WALIOKUWA WAKITOKA KUMSIKILIZA DR MAGUFULI

 Aliyekuwa  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akishuka katika gari la  polisi  baada ya  kufikishwa mahakamani  wakati wa vurugu za machingaji  eneo la mashine tatu  mjini Iringa mwaka  jana(picha na maktaba ya matukiodaima)

Na MatukiodaimaBlog
JESHI  la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani  Iringa watumia mabomu ya machozi kuwakamata wafuasi  zaidi ya 60  wa  chama  cha  Demokrasia  na maendeleo (chadema ) akiwemo mgombea  ubunge wao  jimbo la  Iringa mjini  mchungaji Peter Msigwa matatani  kwa kumpiga mawe mkuu wa kikosi cha  kutuliza ghasia (FFU) Iringa na   wananchi  waliokuwa  wakitoka katika mkutano  wa mgombea  Urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli.

Baada ya  polisi kufatua mabamo mawili ya machozi kwa ajili ya  kusambaratisha  wafuasi hao baadhi yao  walikimbia huku  mgombea  ubunge  huyo Mchungaji Msigwa akienda kujisalimisha mwenyewe  polisi baada ya  kutakiwa  kufanya   hivyo kabla ya  kukamatwa na  polisi.

Imeelezwa  kuwa   wafuasi hao ambao  wengi  wao ni vijana walikuwa  wamekutana katika  eneo la kambi ya  kampeni ya Chadema  iliyopo  eneo la Hoteli  ya  Sambala jirani na kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa  ajili ya kikao cha ndani toka majira ya mchana na jioni  ndipo  walipofanya  vurugu   hizo  wakati wananchi  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za mgombea  huyo wa Urais wa CCM.
Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Rmadhan Mungi aliwaeleza  jana  waandishi wa habari  kuwa tukio  hilo  lilitokea   jana  majira ya saa 12;30   jioni baada  ya  wafuasi hao  kufunga barabara  kuu ya  Iringa –Dodoma  na  kufanya  vurugu  hizo kwa kuwarushia mawe  wananchi  waliokuwa  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za Dr Magufuli uwanja  wa  Samora.
Alisema  kuwa  wakati  jeshi la polisi  likiwa katika mkutano wa mgombea  huyo wa Urais wa CCM walipokea taarifa kuwa  kuna  vijana wa  boda  boda  zaidi ya 150 walikuwa  wakijikusanya  kuelekea  katika eneo hilo la Sambala Lodge  na baada ya kufuatilia ndipo  walibaini  kuwa  wanakwenda katika  kikao chao cha  ndani  na kwa kawaida  jeshi la  polisi halikatazi  watu  kufanya  vikao  vyao vya  ndani .

“Jeshi  la  polisi  halizuii  wanachama wa  chama  chochote cha siasa  kufanya vikao vya ndani kwani  ni haki yao ya  kisheria na kikatiba …..lakini  baada ya  kikao chao kumalizika  vijana hao  walitoka  nje ya ukumbi  huo uliopo kando kando ya  barabara na  kuanza  kufunga  barabara  na kucheza muziki katikakati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine wa barabara  kushindwa  kupita  ……baada ya   vurugu hizo nilimuagiza mkuu wa FFU  kwenda  kuwatoa watu  hao  barabara ila  walipuuza na kuishia kumpiga mawe  na  baadae  kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo ya Sambala  eneo  ambalo  wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za Chadema  “ alisema kamanda Mungi.

Alisema  wakati wa vurugu  hizo baadhi ya  vijana  waliumia kwa  kuruka ukuta  na wengine kwa  kuanguka wakati wa  kujaribu  kukwepa  kukamatwa na  kuwa wale  wote waliokamatwa  watafikishwa mahakamani wakati  wowote  kuanzia  sasa na  kuwa miongoni mwao  yumo mgombea  ubunge  jimbo  hilo Mchungaji Msigwa .

Mbali ya  mchangaji  Msigwa   wengine  waliokamatwa kwa tuhuma  za  vurugu  hizo  ni pamoja na mgombea  udiwani  kata ya  Gangilonga  ambae  pia ni mkuu wa kambi hiyo Dady Igogo
Kamanda  Mungi  alisema  watuhumiwa  wote  watafikishwa mahakamani  wakati wowote  kuanzia sasa mara baada ya upelelezi  kumamilika  alisema  kuwa mchungaji Msigwa hakuwepo katika  eneo la  tukio wakati  vurugu hizo  zikitokea  ila ameingizwa katika  orodha  ya  watuhumiwa kwa  wakosaji wakuu  wapo  makundi manne likiwemo moja la  yule  anaendenda kosa kwa  mikono  yake ,kundi  la  pili  muwezeshaji au  mshauri  na  kundi la nne kutoa hamasa kwa  wakosaji hivyo  alisema mgombea  huyo anashikiliwa kwa kutuma za  kutoa hamasa kwa watuhumiwa hao  kufanya  vurugu.
Wakati  huo  huo jeshi  hilo la  polisi  limepiga marufuku  vyama  vyote  vya  siasa kuwahamasisha wafuasi ama  wanachama  wake  kufanya  vurugu  za wakati  huu  wa kampeni na  kuwa kamwe jeshi  hilo halitamvumilia kiongozi ama mtu  yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani.

“Amani ni  kitu cha kwanza na yeyote anayetishia  kuvuruga amani ya Iringa anatishia kazi  za  polisi Iringa kamwe  hatavumiliwa  zaidi ya  kuchukuliwa hatua kali na kuwataka  vijana  kuepuka  kutumiwa na wanasiasa  kufanya vurugu  “

Kuhusu  mwenendo  wa  kampeni toka  zianze alisema  kuwa  hadi  sasa  tupo  nusu ya kampeni  hizo  toka  zianze na  kuwa  toka  tarehe 22 hadi 30  mwezi wa nane hakukuwa na  kosa  lolote   lililoripotiwa kutokea  kuhusiana na kampeni  ila  tarehe 1 hadi 5 mwezi wa tisa  kulikuwa na makosa 9  yaliyoripotiwa kituoni na  tarehe 5- 19 kulikuwa na makosa 17 yaliyoripotiwa na makosa 15  yalitokea  jimbo la Iringa mjini na makosa mawili  wilaya ya  Mufindi huku katika wilaya ya Kilolo hakuna  kosa hata  moja
Hivyo amewataka  wagombea na  wafuasi wao  kufuata maelekezo  yaliyomo katika kitabu  cha maadili ya uchaguzi kilichotolewa na tume ya Taifa ya  uchaguzi .


Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa katika ukurasa  wake wa fecaboook alithibitisha kukukamatwa kwa  vijana  hao na kiongozi wa kambi  hiyo Bw Igogo wakiwa katika ngome    hiyo ya kampeni.

2 comments:

Anonymous said...

Typical political styles za akina Lema,Sugu, Msigwa za ku - kampeni kwa ku instigate vurugu.

Anonymous said...

Inge kua ccm ungeona wanao jiita wana mabadiliko wanavyotukana na coment zao, ila huyo Msigwa hafai kuwa mchungaji,,,, analaana.