Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika mkutano wake
wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kalangalala
mjini Geita leo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Mgombea
Urais Huyo amewaambia wananchi wa Geita kuwa mara atakapoingia Ikulu,
moja ya changamoto anazotarajiwa kuzipa kipaumbele ni pamoja na suala la
kutatua mgogoro wa wachimbaji madini wadogo wadogo.
Magufuli
ameasema kuwa akiingia madarakani atawapa maeneo wachimbaji wadogo wa
madini nchini ikiwa ni pamoja na kuwakopesha mitaji na kuwapa vifaa vya
kisasa vya kufanyia kazi zao pamoja na mafunzo kwa ajili ya kuboresha
uchimabaji wao ili uwe wa kisasa zaidi na kupandisha kiwango
cha ufanisi wa kazi zao za uchimbaji.
Dkt.
Magufuli leo amehutubia mikutano katika miji ya Runzewe wilayani
Bukombe, Katoro wilayani Chato na Geita mjini akiendelea na kampeni zake
za kwaomba wananchi kumpa kura za ndiyo ili aweze kuingia Ikulu na
kuwafanyia kazi Watanzania kama kiongozi na Amiri Jeshi mkuu wa
Tanzania.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa Geita na vitongoji vyake wakiwe kwenye mkutano wa
kampeni wa Dkt John Pombe Magufuli uliofanyika jioni ya leo mjini humo. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-GEITA
Wananchi
wa mji wa Geita na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa
shule ya msingi ya Kalangalala,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe
Magufuli alipokuwa akijinadi na kumwaga sera zake mbele za wananchi hao
ikiwemo pia na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais kwa kushinda kura nyingi
ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwandani Wagombea Ubunge wa jimbo la Busanda Mh.Lolensia Bukwimba na Dkt Meedad wa Chato mapema mchana huu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita, kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.Dkt Magufuli atahutubia jioni ya leo mjini Geita kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mapema leo mchana kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
Wananchi wa Runzewe wilaya ya Mbongwe mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizinadi sera zake na kuwaomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano,kwenye viwanja vya mnada wa Ng'ombe,katika mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo maelfu ya Wananchi wamehudhuria.
Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi wa Runzewe wakimshangilia Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano
Wakiwa na mabango yao wakishangilia ujio wa Magufuli
Wananchi wa Runzewe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi na kuomba kurra za ushindi ili aweze kuwa Rais wa Tanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana kwa furaha na kijana mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo.
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwapokea mlemavu wa ngozi Albino Lazaro Malendeka kushoto ambaye alikuwa mtumishi wa kikundi cha Red Briged cha Chadema baada ya kujiunga na CCM mjini Geita leo na William Mabula Msalaba aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Geita.
Wananchi wa Katoro wakiushangilia msafara wa Dkt Magufuli alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Msafara wa Mgombea Urais ukielekea kwenye mkutano wa hadhara ndani ya mji Mdogo wa katoro mkoani Geita.
Nyomi
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Geita Mama Fatma Mwasa,pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM mjini Geita wakati wa mkutano wa kampeni leo
Wakazi wa Geita wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.
Wananchi wa Geita mjini wakifuatilia mkutano wa kampeni
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita na mgombea ubunge wa jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku a.k.a King Msukuma akihutubia malefu ya wananchi wa Geita mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Urais,ambapo Ndugu Joseph aliwaomba wakazi wa Geita na vitongoji vyake kumchagua Dkt John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Steven Masele akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa Geita
Nyomi la watu likishangilia
Wananchi wa Geita mjini wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa
Nyakahura,wilaya ya Biharamulo alipokuwa akielekea mkoani Gieta
kuendelea na kampeni zake.


























3 comments:
Huu umati wa watu uliofurika tena katika mji mdogo tu kama ingekuwa ukawa basi wangechonga mpaka asubuhi . Ukawa wanshitaji at least mwaka moja wa kampeni tena CCM wao wasiwe wanafanya kampeni ndio labda wanaweza kushinda ikiwa CCM watamsimamisha mgombea wa kaliba ya magufuli yale maji mapana bana he!
JAMANI AMA KWELI MAGUFULI FIX.ANAJIFANYA KUWASHANGAA WATU WA GEITA KWA KUFIKA KWA WINGI.HASEMI KWAMBA KWANZA MSAFARA WAKE PEKE YAKE WA KWAKE UNA MABASI MAKUBWA HAMSINI, MINI BUS SITINI NA TANO,GARI NDOGO 210.MSAFARA WAKE PEKE YAKE UNAJAZA UWANJA WA MPIRA MPAKA NYOMI.TUENDELEE,ANAZUNGUKA NA KIILA AINA YA WASANII MFANO DIAMOND,ALLY KIBBA.WASANII PEKE YAO YAPATA MIA TATU.ANAJIFANYA KUSHANGAA.MATAGAZO YANAYOPITA KABLA YA MSAFARA KUFIKA YANARUSHWA NA MALORI MAKUBWA YENYE POWERFUL 4-6 SPEAKERS KUMI NA NNE.KWA UJUMLA CCM HAWAMNADI MGOMBEA WAO KIMAADILI YA SIASA,ILA NI KUWAPELEKEA WANANCHI: GRAND FIESTAS ZA MUZIKI AMBAZO HAZIJAWAHI KUTOKEA TANGU TUPATE UHURU-MIAKA 55 ILIYOPITA.MATUMIZI KWA SIKU YAANI GHARAMA BILLION 2.5 JIULIZE:MPAKA MWISHO WA KAMPENI CCM WATAKUA WAMETUMIA TRILLION NGAPI ZA WALIPA KODI? .SASA HIVI HAZINA IMEKAUKA,BENKI KUU IMEKAUKA, CCM INAYADAKIA MAKUSANYO YA TRA MLANGONI. TUNAMUONEA HURUMA RAIS AJAE WA AWAMU YA TANO MHE.EDWARD LOWASSA ATAIKUTA HAZINA NYEUPE,BENKI KUU NYEUPE,MADENI YA NCHI MAPYA NA YA ZAMANI KWA MATRILLION.MUNGU YUPO TUTASAIDIANA NAYE KUUFUFUA UCHUMI WETU HUSUSANI KUCHUKUA HATUA ZA DHARURA MUAFAKA.
Waliofilisika ni Ukawa ndiyo maana mmeanza kuomba michango kwa watu binafsi. Na hiyo idadi ya magari unayoitaja unaijua wewe tu kwa sababu zako binafsi. Watanzania ni watu wenye akili timamu na hata watoto wadogo ambao hawajaanza kuelewa chochote huwezi kuwaongopea hivi. Mwenzetu vipi ndiyo umejua kuandika siku hizi tu na hivyo unatumia fursa hii kufanyia mazoezi na kujifurahisha! Ilani tu kama unatafuta kazi kwenye chama chako hawata kupa kazi kama watakua wanasoma huu uongo unaoandika. Ujue siku hizi waajiri wanakwenda mitandaoni kuangalia jinsi watu wanavyoandika na lugha wanazotumia na kama uko kwenye utafutaji kazi hii inaweza kuwa kasoro kubwa sana.
Post a Comment