MAGUFULI AWASHA MOTO SHINYANGA
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Shinyanga mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM
uliofanyika kwenye uwanja wa Kambarage ambapo aliwaambia wananchi hao
kuwa wakati umefika wa kujenga Tanzania mpya yenye viwanda vya kutosha
kutoa ajira kwa vijana wengi.
Alisema
pia kuwa Serikali yake itakuwa rafiki wa sekta binafsi na kuwajengea
uwezo wafanya biashara ndogo ndogo ili waweze kujiendeleza.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Shinyanga kwenye mkutano wake wa Kampeni ambapo aliwaambai wananchi hao
kuwa serikali yake itakuwa ya kufanya kazi zaidi kwa maendeleo ya nchi.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea
ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele kwenye mkutano
wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya
Kambarage.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia
wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo
aliwaambia wananchi hao Mgombea urais anazo changamoto za Shinyanga
mjini na anaamini atazitatua hivyo amewataka watu wake kumpa kura nyingi
za Dk. John Pombe Magufuli ifikapo tarehe 25 Octoba
Wasanii wakipiga push up jukwaani kabla ya mgombea wa urais kupitia CCM hajahutubia.
Mjumbe
wa Kamati ya Kampeni ya CCM Mzee Samuel Sitta akihutubia wakazi wa mkoa
wa Shinyanga kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM
Dk. John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah
Bulembo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kumnadi
mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea
wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa mji wa
Shinyanga mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa
Kambarage.
Wananchi wa Jimbo la Solwa wakimsikiliza Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
No comments:
Post a Comment