Advertisements

Thursday, September 17, 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AIBUKA NA KIHOJA HIKI LEO,NAYE AUNGANA NA LIPUMBA NA SLAA KUIMBA WIMBO WA LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA


NA KAROLI VINSENT
MWENYEKITI wa cha Democratic Party (DP), Christopher Mtikila ameibuka na kihoja pale alipowataka Watanzania siku ya kupiga kura tarehe 25 octoba mwaka huu kutoipigia kura kipengele cha Urais na wataka watanzania
kuwachagua wabunge na Madiwani peke yake,kwakuwa wagombea wote wa urais waliosiamishwa kwenye vyama vayo hawana uwezo wa kuliongoza taifa hili.
Kauli ya hiyo ya Mchangaji Mtikila ameitoa leo Jijini Dar es Saalam wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema nasafi ya urais inatakiwa kupewa mtu mzalendo na mwenye maono chanya na nchi yake ili aweze kulivusha taifa mahala llipo sasa anapoadi penye shida lukuki akisema wagombea wote wa Urais hawana sifa hizo.
Mchangaji Mtikila huku akiwataka kwa Majina wagombea hao amesema Mgombea wa Chama cha Mapinduzi John Magufuli pamoja na Mgombea wa Urais kupitia Chadema Edward Lowassa ambaye anaungwa mkono na Vyama vya Ukawa akisema wagombea hao hawafai hata kufikiliwa kupewa nchi kwani wanaweza kulifikisha taifa sehemu anayodai ni mbaya.
Amesema kitu ambacho anawataka Watanzania kuwa siku hiyo ya kupiga kura ni wajitokeze kwa wingi na kuwapigia kura madiwani pamoja wabunge na kutompigia kura mgombea yeyote wa Urais.

Sanjari na hayo Mchungaji huyo alitumia mkutano wake huo na wanahabari kumshambulia lowassa huku akiwa hana hata ushahidi ,akidai Lowassa anatumiwa na Rais wa Rwanda Kagame kuja kuleta mchafuko nchini.

No comments: