ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 27, 2015

MWIGULU NCHEMBA AENDELEA KUCHANJA MBUGA,AMALIZA KAZI MKOA WA SINGIDA KUHAKIKISHA CCM INASHINDA KWA KISHINDO

Chopa ya Chama Cha Mapinduzi ikiongozwa na Mjumbe wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi ikipasua ANGA la Mkoa wa Singida hii leo wakati wa kampeni kwenye Majimbo mbalimbali.Mapema leo,Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Igunga Ndg.Dalalary Kamfumu.Mwigulu ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi wa Igunga kuichagua CCM kwenye nafasi zote,Swala la Mabadiliko halinauhusiano na vyama vya siasa,Mabadiliko ni shughuli za Maendeleo,Sehemu ukiona hakuna Umeme pakawekwa Umeme hayo ndio Mabadiliko.Kubadilisha vyama vya siasa tena kwa Upinzani huu wa Tanzania uliobeba Zigo la Walarushwa maarufu Nchini ni kupoteza Muda.
Sehemu ya Mamia ya Wananchi wa Jimbo la Igunga wakifuatilia Mkutano wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi hii leo.Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Jimbo la Igunga mapema hii leo.Mbunge mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi kwa Jimbo la Mkalama Ndg.Allan Kiula akibebwa na Wapiga kura wake kupelekwa eneo la mkutano hii leo.Mbali na kuwa Mkalama hakuna Upinzani wa kuiangusha CCM,Lakini Mwigulu Nchemba alitumia nafasi yake kuwasisitiza Wananchi wa Mkalama kutofanya Uchaguzi kwa Ushabiki,Uchaguzi mkuu ujao ni hatma ya Taifa letu kwa miaka 5 ijayo.Hivyo wote wenye nia njema na Taifa letu waiunge mkono CCM,Wamchague Magufuli,Madiwani na Mbunge wa CCM.Wananchi wa Jimbo la Mkalama kata ya Ndalanga wakionesha Ishara ya kuiunga mkono CCM kwenye Uchaguzi ujao.Comrade Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Jimbo la Singida Magharibi Ndg.Kingu,Katika mkutano huo Mwigulu alisisitiza kuwa Kingu ni kijana ambaye anakiu ya kuwatumikia Wananchi wa Singida Magharibi,Kwa wakati huu ambao taifa linakwenda kwenye Mchakamchaka wa Magufuli wa kuleta maendeleo Mijini na Vijijini,Kingu ni jawabu tosha kwa Maendeleo ya wanasingida wa Magharibi.Wananchi wakiunga mkono Chama cha Mapinduzi kwa kumchagua Mh.Kingu kwenye uchaguzi huu wa October 25.Mbali na Kumnadi Ndg.Kingu,Mwigulu Nchemba alipokea Vijana 23 walioachana na Chadema na kujiunga CCM.Hizi ni baadhi ya kazi za Wananchama wa Cuf na CHADEMA waliojiunga CCM.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa IKUNGI Jimboni kwa Tundu Antipas Lissu hii leo wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wa Chama cha Mapinduzi.Mwigulu Nchemba amewaonya wananchi wa Singida Mashariki kutorudia kosa la kuchagua Upinzani,Kwa muda wa miaka 5 iliyopita Jimbo la Singida Mashariki limekuwa likizo kwenye Shughuli za maendeleo,Hakuna Umeme ,Maji na Barabara ua Miundombinu ya Elimu iliyoongezeka wakati wapinzani walioshika Jimbo hilo.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki kata ya Kaskazini wa Jimbo.Mwigulu NChemba akizungumza na Wananchi wa manyoni,Amewaomba kuichagua CCM kwa nafasi zote,Ilani ya CCM inakwenda kutatua changamoto mbalimbali za jimbo la Manyoni Mashariki.Ilani inatamka wazi kuwa Elimu inakwenda kuwa Bure kwa Darasa la Kwanza hadi la Kidato cha Nne,Pia vijiji vina kwenda kuwezeshwa Milion 50 kwaajili ya Shughuli za Ujasiliamali.Wananchi wa Manyoni Wakifuatilia Mkutano wa hadhara wa kampeni za Chama cha Mapinduzi.Wananchi wa manyoni wakinyoosha Mikono yao kuashiria kura zote kwa Magufuli,Ubunge na Udiwani wa CCM.
Picha na Sanga Festo Jr.

No comments: