ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 26, 2015

MWILI WA MAREHEMU CELINA O. KOMBANI WAWASILI DAR ES SALAAM LEO JIONI

 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukitelemshwa baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina Kombani umewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali . Tutaendelea kuwafahamisha ratiba kila tutapopata taarifa. 
 Familia ya marehemu, viongozi mbalimbali na wananchi wakisubili mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ulipowasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Aliyeshikwa bega wa tatu kushoto ni Mume wa Marehemu Mzee Kombani.
Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipakiwa  kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Picha na Emmanuel Massaka.

No comments: