Yanga ni zaidi ya Mcharo Simba wametepweta baada ya kukubali goli moja kila kipindi alikuwa Tambwe aliandika bao la kwanza dk ya 44 ya kipindi cha kwanza, ikumbukwe kuwa Tambwe alikuwa kipenzi cha wana msimbazi hao na wakampotezea na kunyakuliwa na Yanga. Kipindi cha pili Busungu aliesajiliwa kutoka kwa wafunga buti wa mgambo aliiandikia Yanga bao la 2 dk ya 79. Yanga sasa imefuta uteja uliodumu zaidi ya miaka 5 kila wanavyo kutana na Simbanilikuwa ni kilio tu cha kusanga meno safari hii ni zamu yao Simba kusaga meno hadi ya jacho liwakauke.

No comments:
Post a Comment