Msanii wa bongo fleva, Nay wa Mitego amemvaa mjumbe wa kamati ya Kampeni ya CCM,January Makamba na kudai yeye ni mnunuaji mkuu wa tafiti na wasanii kwa lengo la kukisaidia chama chake.
Nay alimjibu January Makamba aliyepost ujumbe ukionyesha kushangaa tuhuma dhidi ya CCM kuwa imekuwa ikinunua wanasiasa,tafiti pamoja na wasanii kwa lengo la kuulaghai umma.
"Zitto kanunuliwa. Slaa kanunuliwa. Lipumba kanunuliwa. Twaweza imenunuliwa. Synovate imenunuliwa. Wasanii wamenunuliwa. Tuwe creative kidogo" Aliandika January Makamba.
"Ni kabisaa kwani uongo? We ndo mnunuzi mkuu. Bro kama ubunifu ni hela basi we Master wa Ubunifu... @JMakamba Ongeza ubunifu bro" Alijibu Nay wa Mitego

4 comments:
nampenda sana dogo huwa anawachana live tena musiki wake ni poa sana hana usharobaho wa uharo ni kidume kweli wa mbegu. big up nay.natakuelewa tu wakitaka wasitake. wewe ndo dume la mbegu. hana unafikii wa kijinga jinga.
Hakuna chochote cha maana alichosema!
Huyu bwana mdogo anatakiwa kurudi shuleni kwanza kabla ya kubishana na makamba.
There's no substance zaidi ya kuongea siasa za vijiweni.
Post a Comment