mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mufindi Bw Tovick Kahemele akimuombea kura mgombea udiwani kata ya Bomani Bw John Chota kulia
Mgombea ubunge jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi kulia akisalimiana na mmoja kati ya wapiga kura wake
Mgombea ubunge jimbo la Mufindi Kaskazin Bw Mahamudu Mgimwa akiwahutubia wananchi wakati wa mkutano wa Chumi
Mjumbe wa NEC Mufindi Marcelina Mkini akiomba kura za CCM
Mjumbe wa NEC Iringa Mahamudu Madenge akizungumza na wananchi wa jimbo la Mafinga
Na MatukiodaimaBlogMGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mafinga Bw. Cosato Chumi (CCM) amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwa na iamani na kuwa wakimchagua atahakikisha anamulika kwa kutumia tochi ubadhilifu katika sekta za elimu, afya, kilimo, barabara, maji na kuhakikisha kuwa hakuna fedha ambazo zitatolewa na serikali kuleta maendeleo kwa wananchi zitaliwa na watendaji ndani ya jimbo la Mafinga.
Hayo ameyasema jana wakati alipokuwa akijinadi kwa wananchi wa jimbo la Mafinga katika Mtaa wa Bomani ambapo pia ulifanyika uzinduzi wa kampeni za udiwani katika kata hiyo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu pamoja na madiwani wote ambao wametangaza nia ya kuwania nafasi zao katika jimbo hilo la Mafinga Mjini.
Bw. Cosato Chumi alisema kuwa wananchi wa jimbo la Mafinga ni mashahidi wa shida zinazowapata na kuwakera wananchi ndani ya jimbo la Mafinga Mjini ambapo alisema kuwa Hospitali ya wilaya kutokana na kuzidiwa na wagonjwa atahakikisha kuwa anapigania ili kila kata kuwe na zahanati na katika tarafa za ndani ya Mafinga kujengwe kituo cha Afya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa.
Bw. Chumi aliongeza kuwa atapigania ili madawa na mahitaji yote ya msingi kwa wananchi hususani wagonjwa kuwa yapatikane na kuhudumia wananchi ambao kwa sasa kutokana na mlundikano mkubwa wa wagonjwa katika Hospitali ya wilaya wagonjwa wanapoteza muda mwingi katika kutafuta matibabu ya afya zao na familia zao.
“Nitahakikisha kuwa pesa zote za Umma za maendeleo zinasimamiwa kikamilifu na hakuna ufujaji wa aina yoyote ile ambao utatokea na kuongeza kuwa fedha zote zitakazotolewa ndani ya mfuko wa jimbo, pesa za serikali za maendeleo pamoja na miradi mbalimbali zitamulikwa kwa umakini ili zitekeleze shughuli ambayo imelengwa”, alisisitiza Bw. Chumi.
Alisema kuwa endapo viongozi wanategemea sana utendaji wa kazi na shughuli za viongozi kutokana na kuwepo kwa umoja na mshikamano ambapo alisema kuwa shule za sekondari zitahakikisha kuwa zinaendelezwa kila kata na kuwahakikishia wananchi hususani watoto wao wanapata elimu sahihi.
Aidha, alisema kuwa mabweni katika shule za sekondari yatahakikisha kuwa yanajengwa kwa malengo ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanatulia shuleni na kusoma kwa utulivu ambapo alisema kuwa sekta ya elimu inatakiwa ipewe kipaumbele ili watanzania wote waelimike na kuwezeshwa kujitegemea na kujiajiri na kuajiriwa na sekta za binafsi na serikali kwa manufaa ya kukuza uchumi ndani ya nchi.
Akizungumzia suala la kushughulikia usalama, Bw. Chumi alisema kuwa atahakikisha kuwa anapigania kila kata ndani ya jimbo la Mafinga linajengewa kituo cha Polisi ili kuwasaidia wananchi kulinda usalama na mali zao, kuwasaidia wananchi endapo watahitaji misaada ya haraka kutoka kwa sekta ya ulinzi wa jeshi la polisi ikiwemo mwananchi akipata ajali, akiibiwa, akivamiwa na kupata misukosuko ya aina yoyote ile ambayo itahitaji jeshi la polisi kuingilia kati kushughulikiwa kwa haraka.
Mwisho;
No comments:
Post a Comment