Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL
kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es
Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu
mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano
(500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo
dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji
wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi
laki tano.
Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika
mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na
Mbuyu Twite.
Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki
tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC
mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC
dhidi ya mwamuzi.
Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu
hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji
ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui
uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union
kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa
nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa lugha ya matusi kwa waamuzi
na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii
Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba
msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji
Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda
uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa
kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili
(200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar
uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe
watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote
zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports
kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu
za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu
wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi
mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa
Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza
wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi
wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na
kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu
huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.
No comments:
Post a Comment