ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 23, 2015

PUSH UP ZA DK MAGUFULI ZAWA GUMZO NCHINI

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akionesha umahiri wa afya yake kwa kufanya mazoezi ya Push Up wakati wa mkutano wa kampeni mjini Karagwe, mkoani Kagera leo.



 Dk Magufuli akihutubia na kujinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni mjini Nkwenda, wilayani Kyerwa, mkoani Kagera.
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba za Dk Magufuli na ahadi alizokuwa anazitoa.

 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kyerwa, Swisbert Ntambuka wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo leo.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli akijinadi katika Mji wa Nkwenda Jimbo la Kyerwa

 Dk Magufuli akijinadi katika moja ya mikutano midogo midogo jimboni Kyerwa, Kagera
 Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya POosta ya Zamani mjini Ngara leo

 Mgombea ubunge Jimbo la Nkenge, Balozi Diodorus Kamara akijinadi kwa wananchi wilayani Missenyi, Kagera.
 Dk Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akijinadi wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Kyerwa, Kagera
 Mrembo akionesha tabasamu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika wilayani Misenyi, Jimbo la Nkenge.
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wilayani Karagwe leo
 Picha ya Dk Magufuli ikiwa imewekwa kwenye moja ya matairi ya Lori mjini Karagwe
 Ni furaha iliyoje kwa wananchi hawa baada ya kurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli kwamba akishinda urais Elimu itakuwa ya bure kuanzia darasa la kwanza hadi  sekondari.
 Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Karagwe kupitia CCM, Innocent Bilakatwe wakati wa mkutano wa kampeni mjini Karagwe leo
Mke wa mgombea ubunge Jimbo la Karagwe, Jennifer akitumia simu kupiga picha wakati mumewe akinadiwa na Dk Magufuli mjini Karagwe leo.

14 comments:

Anonymous said...

Tufike mahali iwe ni mandatory kwa wagombea nafasi hii kubwa kabisa nchini kuwasilisha their medical records kwenye tume ya uchaguzi kabla hawajaidhinishwa ili kuepuka ya Satta wa Zambia.

Anonymous said...

Lol i bet my man Lowasa can do that with one hand. We need that to happen during the coming presidential debate session as one of the winning point how about that?

Anonymous said...

Watu wengine
Umesikia watanzania tunataka push up zako
Tunahitaji busara zako , bora nenda jeshini au security card Watu wasio Tumia kichwa hutumia miili yako
Umeishiwa hoja
Kwani push up ndo uzima pole

Anonymous said...

Hata ukiruka kichura chura
Wala hatujalishi
Kwani Umesikia urais maguvu umeishiwa hoja na kufikiri
Utajilinganisha na kila kitu kwa Lowassa
Lakini humpati kwa mvua Wala jua
Na ndo chaguo letu
Na goli la mkono lishaanza kuwatudia Mtama

Anonymous said...

NAJARIBU KUTAFUTA TAFSIRI NASHINDWA,NADHANI HII NI MARA YA KWANZA DUNIANI KUTOKEA,YAANI MGOMBEA URAIS CHEO CHA SIASA CHA JUU KABISA KATIKA NCHI,CHEO KINACHOHITAJI HESHIMA,HEKIMA NA UVUMILIVU ANAPATIKANA MGOMBEA ANAYEJINADI KUWA TAYARI KWA SHARI,TENA MBELE YA UMMA WA WATU ANATUNISHA MISULI,ANATAMBA NA PUSH UP, ZA MAZOEZI YA GYM KAMA KWAMBA ANAJIANDAA KWA PAMBANO LA MIELEKA NA AU BOXING.MWENYE MAMLAKA YA KUKUPA NGUVU,AFYA NJEMA,PUMZI,NI MWENYEZI MUNGU PEKE YAKE.ANGALIA LEO UKO FIT LAKINI,KESHO UPO HOOOI KITANDANI,HUJIWEZI WA KUGEUZWA.UKIULIZWA KULIKONI HUWEZI KUJIBU UNALIA.AFYA ZETU NI MIPANGO YA MWENYEZI MUNGU TUSIZIFANYIE TAMBO.UNANIKEJELI SAWA WEWE UMEZALIWA SUPER NATURAL? TUNASHUHUDIA WANGAPI WENZETU WANAKUFA BILA KUUMWA,BILA KUOMBA HATA ILE PANADOL YA KUTULIZA MAUMIVU.WAOMBOLEZAJI TUNALIA TUKIULIZWA ALIUGUA NINI TANGU LINI,TUNAJIBU:YAANI AMEFARIKI NA AFYA YAKE,HAKUWAHI KULALAMIKA KUWA ANAUMWA CHOCHOTE KIFO CHA GHAFLA TUU.AFYA,UZIMA, MIPANGO YA MUNGU.MARADHI KIFO,MIPANGO YA MUNGU.TUNAWALAANI SANA WAPAMBE WA MHE.MAGUFULI WALIOMPELEKESHA BWANA HUYU AJISAHAU KWAMBA HII LEO SI HIYO KESHO,KUPATA KUNA MUNGU NA KUKOSA KUNA MUNGU PIA.NI TUKIO LA AIBU KUBWA NA FEDHEHA.NI UCHOKOZI KWA MUUMBA WETU,NA,HAYA,SIJUI,HATUJUI.WACHENI MUNGU AITWE MUNGU.

Anonymous said...

Kampeni
Kaanza na kupiga ngoma, kucheza muziki jukwaani
Na push up juu
Ukiwa rais itakuwaje?
Urais hufai 10000000 % unafaa kuwa mtendaji tu magufuli ushauri WA bure
CCM na mafisadi wake wanakutumia we we wafanikishe mambo Yao
Lakini 25 October
Lowassa Lowassa

Anonymous said...

kweli kabisa,wapambe wanampelekesha magufuli kufanya vitu vya ajabu kabisa,aliwahi kuliona wapi hilila kupiga push up jukwaani kama mgombea,wapi magufuli wapi kumbe wewe ni out of nuts eeh.tuanzie watangulizi wake mwalimu,mwinyi,mkapa na kikwete.aliona wapi magufuli labda tuwaulize na twende kwa majirani wetu waliotuzunguka kenya,uganda congo,rwanda,burundi,zambia,malawi,msumbiji,swaziland,zimbabwe,lesotho,namibia,south africa angola,naomba nisiendelee nina hasira sana za masikitiko.magufuli anafanya kejeli, uchokozi wa makusudi kwa muumba wetu mwenye enzi,nawaambieni si muda mrefu mjiandae kumdaka kama tufe kama mchezo wa sinema vile.acheni hizo,mwogopeni mungu.anayetaka kuniuliza ruksa.na bado ninayo mengi ya kusema.

Unknown said...

Kabisa alichokifanya magufuli walahi kama yupo ulaya, afya kwanza kuliko kitu chochote na kitendo chake cha kuonesha kwa vitendo umuhimu wa mazoezi na faida zake kwa afya mwanadamu kwa kweli ni mtu wa aina yake. Nafikiri katika kampeni zake atilie mkazo suala la kujenga vituo vya mazoezi nchi zima. Mr magufuli kama ujumbe huu utakufikia tunakupongeza kwa kuonyesha kwa vitendo umuhimu wa mazoezi katika kumletea mwadamu njema. Mazoezi yanafaida nyingi hasa push up ambayo mtu anaweza kufanya wakati wowote na hahihitaji big amount of space. La kushangaza wanatokea wagonjwa wa akili eti mtu kufanya mazoezi ni ishara ya ugomvi mijitu kama hii hatushangai kwanini yanamsapoti lowasa. Eti wanalalamika kuwa kiongozi wa kisiasa tena anaegombea uraisi kufanya mazoezi ni aibu? Jamani

Anonymous said...

TUNA IMANI UJUMBE UMEMFIKIA MGOMBEA MHE. MAGUFULI,WAPAMBE NJAA WAOGOPE KAMA UKOMA MZEE MAGUFULI,IPO SIKU WATAKWAMBIA SASA VUA SHATI LAKO WATU WAONE MISULI,HALAFU SIKU VUA FULANA WATU WAONE MANYOYA,SIJUI MNANIELEWA,HAYA MATUMBO YETU YA ZAMANI UKARABATI KIBAO SI TUTAJAWALAANI WANETU NA WAJUKUU,MNANIELEWA?LOWASSA OYEEE.TUNA IMANI NA LOWASSA,NA NI;LOWASSA PEKEE.

Anonymous said...

Sallen wacha ushamba wewe nipo ughaibuni miaka
Mingi sana sijawahi Wala sijaona wala kusikia mgombea urais apige push up kwenye kampeni jukwaani
Hayo hufanywa na mabondia, wapiga misuli , mabaunza , walinzi WA milangoni
Yote hii CCM wamezoea vijembe , yaani sielewi kwani kwangu mimi vijembe na rusha roho ni kwa wanawake.
Lakini imekuwa ni tabia ya CCM hata kwa wanaume.
Mshindeni Lowassa kwa hoja na si vijembe vya kijinga.
Hata akiwa mgonjwa ni chaguo letu kwanini wazima
Subirini 25octber
Mungu akupe afya njema na maisha marefu Lowassa amen

Anonymous said...

Sallen nakubaliana na wewe kabisa kuwa afya ni kitu muhimu sana kwani afya dhaifa hupunguza kasi ya utendaji kazi kwa mtu yeyote. Nashangaa hawa ndugu zetu wanavyomkandia mgombea urais Magufuli wa CCM kuonyesha kwa vitendo kuwa ana afya bora na hivyo yuko katika hali nzuri ya kukabiliana na shughuli nyingi za kuliongoza taifa kama chama tawala kitarudishwa tena madarakani. Lazima wananchi wenzetu tutambue kuwa kazi ya urais siyo kazi ya lele mama. Ni kazi ngumu ambayo mikiki mikiki yake wakati mwingine ina mtaka mheshimiwa huyo kutolala usingizi wa kawaida kama ambavyo wengine tumuzoea, kusafiri kutumia usafiri wa kila aina wakati akitembelea sehemu mbambali ambapo zingine ziko katika mazingira magumu na kadhalika.

Kama Sallen alivyoeleza hapo juu, Watanzania kwa ujumla wetu huu badala ya kumkandia Magufuli kwa “push up” alizozifanya tungechukua mfano wake huu kama motisha yetu wote kufanya mazaoezi ili kila mmoja wetu awe katika hali nzuri. Maswala ya kifo hawa wezentu waliyoandika hapa hayana maana kwa vile hayo maswala yote yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu lakini vile vile ni Mwenyezi Mungu huyu huyu ametupa akili za kufikiri ili tujilinde na mazingira au vifo ambavyo vinatuandama kabla ya wakati wake. Kwa mfano Mwenyezi Mungu ametupa uwezo na utalaam wa kugundua dawa mbalimbali na njia nyingi za kuweza kujilinda na magonjwa na vifo ambavyo tunaweza kuviepuka.

Pamoja na haya yote, viongozi kuonekana kwenye majukwaa kuonyesha kuwa afya zao ni imara siyo jambo geni. Ukitafuta kwenye mtandao utakuta kwa mfano habari za aliyekuwa mgombea wa urais wa Marekani kwa jina la Mitt Romney hivi majuzi tu aliingia ulingoni na bingwa mstaafu wa masumbwi duniani, Evander Hollyfield na kuzichapa. Mgombea huyu hajawa mwana masumbwi lakini aliingia ulingoni tu kuthibitisha kuwa yeye ni imara na afya yake nzuri. Pamoja na hali hii hakuna mtu amemlalamikia au kumkejeli kiongozi huyu kwa zoezi alilolifanya. Je mpo!

Anonymous said...

Mgombea wetu afya mgogoro.Jitihada nyingi zinatumika kufikia ukweli huo,ni busara watanzania wakajiuliza nini kiko behind all these?
CCM imeomba mdahalo kati ya wagombea,ili impinge kwa hoja,lakini Mbatia anasema ahojiwe yeye kwaniaba ya Lowasa,Does this make sense to yo at all?

Anonymous said...

MITTY ROMNEY AZICHAPE NA EVANDER WE MWEHU NINI,NASEMA UMEWEHUKA AU UMEANZA KUWEHUKA KAMA MHESHIMIWA.ACHA UCHAFU WA MAWAZO ,NADHANI HATA WEWE NI MCHAFU WA NGUO NA MWILI.UOGE AKILI IRUDI

Anonymous said...

Anonymous wa September 24, 2015 at 12:58 PM.

Badala ya kubishana na kutoa matusi ni busara uingie kwenye internet na ku-google kama nilivyoukuezea. Wengine hatuna hulka ya uongo wala matusi. Kama hutakuta picha za hao jamaa leta email yako nitatao nakala halafu nikutumie.