Fredrick Sumaye
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema kama Lowassa atafanikiwa kuingia madarakani Watanzania walioficha fedha nje ya nchi watazirudisha.Sumaye alitoa kauli hiyo jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini Nzega, Mkoa wa Tabora.
Kwa mujibu wa Sumaye, fedha hizo ambazo Serikali ya CCM imeshindwa kuzirudisha zitatakiwa kurudi kwa sababu ni mali ya Watanzania.
“Jana (juzi) mmemsikia Magufuli (Mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli), akisema atakapoingia madarakani atarudisha mashamba ya wananchi yaliyoporwa.
“Kwanza kabisa namwambia Magufuli kwamba Ikulu haingii, lakini sisi tutakapoingia madarakani tutahakikisha walioiba fedha za Watanzania na kuzificha huko Ulaya au Uswisi wanazirudisha,” alisema Sumaye.
Sumaye pia alizungumzia suala la rushwa nchini na kusema kama CCM wangekuwa waungwana wasingemsimamisha mtu yeyote kugombea urais kwa sababu wameshindwa kuwaletea maisha bora Watanzania.
“Magufuli anasema akiingia madarakani atakomesha rushwa sasa kama ana uwezo huo kwa nini ameshindwa kuikomesha wakati na yeye ni waziri katika Serikali iliyokithiri kwa rushwa?
“Magufuli anasema akiingia madarakani atakuza uchumi, kama kweli ana uwezo wa kukuza uchumi kwa nini ameshindwa kuukuza kupitia Serikali ya CCM ambayo yeye ni waziri?
“Magufuli hana lolote, msimchague kwa sababu ameshiriki kununua feri mbovu inayotoka Bagamoyo kwenda Dar es Salaam,” alisema Sumaye.
Katika maelezo yake, Sumaye alizungumzia pia taarifa za viongozi wa CCM wanaodaiwa kuwatisha wananchi wasimchague Lowassa kwa kisingizio kwamba nchi itaingia katika vita kama ilivyotokea Libya na katika nchi nyingine za Afrika Kaskazini.
Sumaye alisema hakuna vita itakayotokea wapinzani watakapoingia madarakani na kwamba vita hiyo itatokea kama Serikali ya CCM haitataka kuondoka madarakani.
kwa habari zaidi za maendelea na siasa pale Tanzania tembelea blog hii.www.simamia.com
kwa habari zaidi za maendelea na siasa pale Tanzania tembelea blog hii.www.simamia.com

8 comments:
AsanteƱi. Msomi wa Harvard huyo.
Wewe Sumaye kweli huoni aibu kuwalahi watanzania pesa gani zilizofichwa unazozizungumzia wakati wewe mwenyewe binafsi ni miongoni mwa waliotorosha mabilioni ya watanzania nje ya nchi. Kwanza kabla ya kuzungumzia pesa za nje rejesha ardhi yote na mali nyengine ulioipora wakati ukiwa waziri mkuu. Mtake msitake wewe na mafisadi wenzio mjiandae kuikabili mikondo ya sheria mara tu magufuli atakapoingia madarakani maana mahakama maalum ya kushughulikia mafisadi tayari imeshakuwa katika mchakato wake mara tu magufuli atakapoingia madarakani iwe tayari kwa kufanya Kazi na hakuna wa kumzuia magufuli kuingia ikulu hiyo taaluma yenu ya ufisadi haitafua dafu lazima CCM itashinda tena kwa kishindo cha radi.
Makubwa mwaka huu
Lakini yote Ukawa tuuu
MZEE SUMAYE,UMEWAGUSA HAO UNAONA MREJESHO HUO WA KIWENDAWAZIMU.SIO YEYE SEPT 8,2015 ;12;44 AM BALI NI MZUKA WA SHETANI WAKE.MBONA BADO MWEZI NA NUSU TUU.ORODHA INAJULIKANA TUNAIJUA ILA SASA PIA KAONGEZEKA BWANA MDOGO MMOJA ATAKUJA KUSEMA MWENYEWE ATAKAPOKUJA KUHOJIWA NA POLISI[HAWA HAWA WATAWAPIGA U-TURN] KWAMBA PESA ZILE ALIZOFICHA NJE NI ZAKE AU ALITUMWA.MZEE SUMAYE CHAPA KAZI BOMOA, FYAGIA, UMBUA NA SASA HIVI WAKIKUONA UMESIMAMA KWENYE JUKWAA PRESHA ZAO AIDHA ZINAPANDA MNO AU WANAAMUA KWENDA KWENYE MABAA KUJILIWAZA MSONGO WA MAWAZO .YAMEWAFIKA
Anony 2:46 AM umesema Sumaye ni fisadi, na kachukua ardhi ni mara 10, ya huyo anachukua mashamba na kulima mazao na kuongeza ajira. Sasa CCM kuuza Tembo na Twiga nje, Escrow hela za stanbic zilichukuliwa na sumaye. Huyu makufuli anaropoka tu hiyo mahakama akawafungulie CCM wenzake.
Njaa at work. .
Sasa mtu unaongea mambo ya mahakama ya mafisadi kama Kufuli ikiingia ikulu! Wewe unamaana gani? Ufisadi upo ndani ya CCM ni lini nani wewe unayemjua aliwahi Kuwa waziri na akapelekwa jela kwa kuwa ufisadi chini ya serikali ya CCM. utasikia kesi iPo alafufu zinapotelea/ zinaishia chini kwa chini. Imepita miaka 50 chini ya chama cha CCM! Enough is enough time to let some body else try to lead our country, 50 and more was good enough for you, your friends and love ones CCM, we tired of been treated like kids na maabunuasi, you all rich and got what you all want from this country(Tanzania) time for you CCM and you compadres to GO. Amen
Pale turiani Mkuu wa nchi mstaafu analo shamba-pori ekari 2500 na mgombea wa ccm alipopita wilaya ya Mvomero katika ziara ya kampeni alipambana na mabango ya wananchi wakimtaka atoe majibu ya lile shamba pori .Wananchi walivyoona halitolei tamko hilo wakaanza kupaza sauti'Tunataka Majibu'mgombea akalikwepa hilo na mshehereshaji akafunga mkutano.NI EKARI 2500 shamba-pori la Mstaafu Mkuu wa Nchi.unajua unafiki mkubwa wa CCM sasa umefikia tamati Buriani yao tarehe 25 Octoba 2015
Post a Comment