TAARIFA YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA JUMUIYA
YA WATANZANIA NEW YORK.
Tunapenda kuwataarifu kuwa tarehe 10 September Viongozi wa jumuiya
tulifanya kikao na walezi wetu(Mabalozi)hapo ubalozini kujadili namna
bora ya kuhitimisha muda wetu wa Uongozi.Kikao hicho kiliazimia mambo
yafuatayo :
A)Kuitisha mkutano Mkuu wa jumuiya hapo tarehe 5 Disemba 2015 ambao
pamoja na mambo mengine utachagua Bodi ya Wadhamini wa jumuiya ambayo
itasimamia uchaguzi ujao wa Viongozi.
B) Viongozi wa jumuiya waendelee kushika dhamana zao wasubiri
kuzikabidhi rasmi kwa Viongozi wapya watakaoteuliwa.Ukumbi wa Mkutano
Mkuu utatangazwa hapo baadae.
Ni imani yetu wakati ukifika Wanajumuiya watajitokeza kwa wingi kuomba
nafasi za uongozi zitakazotangazwa hapo baadae lakini pia tunawaomba
mshiriki kwa wingi katika mkutano Mkuu wa jumuiya utakaofanyika tarehe
5 Disemba.
Viongozi wa jumuiya tunawashukuru Wanajumuiya wote kwa ushirikiano
mnaoendelea kutupa katika kuimarisha jumuiya yetu kwa
pamoja.Tunaushukuru kwa dhati Uongozi wa Ubalozi wetu wa kudumu katika
umoja wa Mataifa kwa mashirikiano yao bila ya kuchoka katika
kuhakikisha tunaendeleza umoja wetu wa Watanzania hapa ughaibuni.
Uongozi
Jumuiya ya watanzania New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania.

No comments:
Post a Comment