ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 24, 2015

TOROKA UJE RASMI KUANZIA LEO WANA UKAWA(30 Days Movement). Makamanda 30 Kuongoza Mashambulizi..


TOROKA UJE RASMI KUANZIA KESHO WANA UKAWA.
Chopa za Kutosha Angani katika kila kanda zikiongozwa na Makamanda 30.
Hii ni operation maalum iliyopewa jina "TOROKA UJE" -Itakayo pita kwenye kata na vijiji , makamanda wa ukombozi watasambaa nchi nzima ndani ya siku 30 vijijini ili kuhakikisha kwamba CCM wanaondoka madarakani oktoba 25. 
Hizo chopa zimegawanyika kikanda 
Lindi , Mtwara na Pwani hii kanda ya pwani itabeba ujumbe okoa gesi yako sasa( itaongozwa na Tambwe Hiza , ). 
Ruvuma, Mbeya na Iringa kanda ya kusini (itaongozwa na Sugu na Msigwa.) .
Kanda ya kati Dodoma , Singida na Morogoro ( itaongozwa na Lissu ) kanda ya ziwa itaongozwa na makamanda sita .
Kanda ya kaskazini itaongozwa na kamanda Ndesamburo akiwa na makamanda sita.
Kanda ya magharibi itaongozwa na Kafulila na 
Kanda ya pwani kati yenye mikoa ya Dar na Tanga itaongozwa na Kubenea , Mnyika na Mdee.

3 comments:

Anonymous said...

NDIYO, HII OPERATION 'TOROKA UJE'NI OPERATION FUNGA KAZI,TUNA IMANI KUA MASHAMBULIZI HAYA YA SIKU THELATHINI[30] YATAKUA FUNGA KAZI.WATAFIKIWA WATANZANIA WENGI ZAIDI,WATAPATA UFAHAMU NA UELEWA MPANA ZAIDI,WALE AMBAO KWA BAHATI MBAYA MPAKA SASA BADO WAPO MIKONONI MWA MASALIA YA MWISHO NDANI YA CCM WATABADIRIKA NA, HII AKILI MPYA,MWELEKEO MPYA NDIVYO HATIMAYE VITAKAVYOMNYANYUA NA KUMPA USHINDI MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA UKAWA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA,WABUNGE NA MADIWANI.SASA HIVI TUMEFIKIA NA TUNAUSOMA USHINDI WA ASILIMIA THEMANINI NA MBILI [82%]HII PUSH MPYA YAANI MAJOR SLAUGHT ITAIONGEZEA UKAWA BINGO TUNA UHAKIKA ASILIMIA MPYA NANE[8%] NA HIVYO USHINDI WA MHESHIMIWA LOWASSA KUFIKA ASILIMIA TISINI [90%]YAANI KWA USHINDI HUU KAMA VILE UCHAGUZI WA CHAMA KIMOJA WA KURA ZA NDIO AU HAPANA.JAMANI UKAWA RAHA.

Anonymous said...

Ndoto za alinacha. Kwa nini msiandike kuwa ushindi mtapata asili mia 120 kama ilivyo spidi yenu mliotutangazia hivi karibuni? Mimi na wengine wa aina yangu tunaopenda mwendo wa pole pole tutabaki CCM yetu tu hata mkizunguka nchi nzima mara 10. Kwa vile hela zimewaishia sasa ndiyo mnaona umuhimu wa kwenda na magari! Hizo hela mlioanza kuchangisha sasa sijui mtazirudisha lini na vipi! Mjue Ikulu sio mahali pa biashara baba wa taifa alishasema na kuwa wale wanaofikiria kwenda huko kwa lengo hilo wajue kuwa pale sio mahala pao. Mna kazi kubwa na ngumu bado inawasubiri.

Anonymous said...

Ukawa kushindana na CCM hasa katika suala linalo husisha matumizi ya pesa ni kutafuta kujimaliza . CCM ipo miaka nenda rudi ipo vizuri sana kiuchumi ukilinganisha na wao, CCM inamarafiki wa damu kabisa wenye nguvu kama chinese communist party achilia mbali akina ANC south African. Ukawa bila ya ridhaa ya watanzania wenyewe kuamua kuwa sasa wakati umefika kuikabidhi nchi kwa wapinzani basi mpaka kiama hawawezi kushindana nguvu na CCM. Hakuna wakati ambao ukawa wanamuhitaji dk slaa kama sasa. Kwa upande wa CCM watakuwa wapumbavu kama watashindwa kuwatumia Dk slaa na Prof Ibrahim lipumba katika kipindi hiki cha lala salama .Kama ningekuwa a campaign master mind wa CCM basi ningewapa ajira dk slaa na lipumba haraka haraka kwa harama yeyote ile to bring the last blow in ukawa head. Dk slaa na Prof Ibrahim lipumba ni muhimu kwa sasa kuja kuwaelimisha watanzania hadaa zinazotumiwa na akina Mbowe na wenzake wa ukawa kuwalaghi watanzania kwa kuwahadaa na ahadi za mabadiliko hewa. Lengo la Lowasa na wapambe wake wa ukawa sio mabadiliko ya maendeleo ya nchi bali ni kuhakikisha wanaingia ikulu kwa harama zozote zile na kwambia uchaguzi huu ukipita salama basi watanzania washukuru sana kwani ukawa wanaamini liwe lisiwe lazima waingie ikulu hata kwa nguvu hata wakija kushindwa kihalali wameshaeka zana yakwamba watakuwa wameibiwa kura sasa hiyo si dalili nzuri kwa Tanzania . Lowasa mtu wa matempa, Mbowe mtu wa matempa, Tundu Lisu ndio usiseme kabisa, Sumaye manongwa yaani hakuna watu wa busara kule ukawa ni bomb linalokaribia kuripuka watanzania wawe makini sana na hawa watu isiwe wanawashibikia tu bila ya kufikiria athari zake.