ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 17, 2015

TWITTER ZA DR MAGUFULI JITITIRISHE

  1. Ulinzi na Usalama: Tutapambana na changamoto kubwa likiwemo jukumu la kudumisha amani na utulivu.
  2. Tutajenga barabara za Nyahua-Chaya(km 85),Urambo – Kaliua(km 33) na Chagu – Kazilambwa(Kigoma/Tabora )(km 40) kuiunganisha Tabora na Kigoma.
  3. Tutaunda Serikali yenye nidhamu na uwajibikaji na rafiki wa wafanyakazi sanjari na kuboresha mishahara/marupurupu.
  4. Mwaka 1978 - nikiwa na umri wa miaka 19, Kidato cha Nne katika shule ya Sekondari ya Lake, Mwanza.
  5. Shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji - Kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopa.

  6. Nimefikishiwa kero kwa mabango yenye ujumbe wa aina mbalimbali. Ilani ya CCM ni njia pekee yenye kutatua kero hizo.
  7.   retweeted
    Pongezi kwa Sheikh Aboubakar Zuberi kwa kuchaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania. Mungu amjalie hekima na afya katika kutimiza majukumu yake.
  8. Wananchi Mkoa wa Simiyu ni wafugaji na wakulima wakubwa wa zao la pamba- tutasimamia upya sekta hii ili iwe na tija.
  9. Nakumbuka mwaka 1995, Mzee Mkapa alipita Chato kuniombea kura na ndiyo ukawa mwanzo wangu kuingia katika siasa.
  10.   retweeted
    Jeshi la Kujenga Taifa, Makutopora mwaka 1983. akiwa na miaka 24, katika mafunzo ya kijeshi.
  11. Hakika sitawasahau wananchi wa Mkoa wa Mara kwa namna walivyonipokea nilipopita kuinadi Ilani ya CCM. SITAWAANGUSHA!
  12. Nikiwa Butiama, nimepata heshima kubwa ya kupewa kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
  13. Nitaitekeleza Ilani ya CCM "Ukurasa kwa Ukurasa"- nimefanya Mkutano Butiama na kutembelea kaburi la Baba wa Taifa.
  14.   retweeted
    Yesterday I had the pleasure of welcoming , the next President of Tanzania, in my constituency.
  15. Nimehitimisha kampeni Mkoani Tanga, ahadi kubwa ni kuufanya tena Mji wa Tanga kuwa wa Viwanda ikiwemo kuvifufua vilivyokufa. ASANTENI TANGA.
  16. Barabara ya Soni hadi Bumbuli (km 22) ina jiografia ngumu ya mawasiliano, tutaijenga kwa kiwango cha lami - Bumbuli.
  17. Natambua Tanga ulikuwa Mji wa Viwanda, bahati mbaya viwanda hivyo vimebaki kuwa magofu - serikali yangu itavifufua.
  18. Serikali ya Awamu ya Tano - Elimu ya bure kuanzia darasa la kwanza hadi Kidato cha Nne.
  19. Wananchi wamekuwa wakinipokea na mabango wakinitaka niwatatulie kero zao, yote hayo nitayasimamia - Mvomero.
  20. Morogoro - sitamuonea mtu, ila nitafuta mashamba pori yaliyotelekezwa au kutoendelezwa ili yagawiwe kwa wananchi.
  21. Kampeni Ifakara, nimepata mapokezi makubwa. Nitatatua tatizo sugu la ugomvi kati ya wakulima na wafugaji.
  22. Barabara ya Dodoma – Manyoni (km 127) na Manyoni – Singida (km 118) kabla na baada ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
  23.   retweeted
    1991 Chuo Kikuu - Dar, kushoto akifanya Shahada ya Uzamili - Kemia. Kulia ni rafikiye, Christopher Kadio.
  24.   retweeted
    Dokta akiongea na Husna Mikidadi, binti mwenye ualbino wakati akimalizia mkutano wake Mtwara jana jioni.
  25. Tangu nianze kampeni nimetembea kwa barabara takriban kilomita 4885 lengo nijumuike na wananchi ili nijue kero na changamoto zinazowakabiri.
  26. Tutakamilisha ukarabati na ujenzi kwa kiwango cha lami unaoendelea/umekwishaanza barabara ya Mtwara hadi Mbamba Bay
  27. Serikali nitakayoingoza itaendelea kuwalinda na kuwatambua Walemavu wote nchini ikiwemo kukomesha kabisa mila potofu.
  28. "Halmashauri zitahakikisha wazee wanatambuliwa na kupewa matibabu bure katika hospitali za Serikali"ILANI YA CCM 2015
  29. Nimeendelea na kampeni mkoani Mbeya, tumepata mapokezi makubwa Jijini Mbeya. Wananchi wananiamini na kuiamini CCM.
  30. Nimefanya kampeni Makongolosi na Chunya na nikafanikiwa kusafiri kupitia barabara ya Makongolosi hadi Chunya (km 36).
  31. Nawashukuru wananchi wa Mbalizi kwa kuniamini na kukiamini Chama cha Mapinduzi ili kiendelee kushika dola.
  32. Nimefarijika kuona wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma wameendelea kuniamini na kukiamini Chama cha Mapinduzi.
  33. Nimepata mapokezi makubwa ya kihistoria Mkoani Rukwa, asanteni sana. Ahadi, tutamalizia ujenzi wa barabara kutoka Sumbawanga hadi Kigoma.
  34. Nawashukuru wananchi wa Mpanda kwa kuniunga mkono nilipopita kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
  35. Leo tarehe 23 Agosti 2015 , nitaongea na watanzania namna nitakavyoitekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa vitendo.
  36. Mwaka 2004 niliwaahidi watanzania watasafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwa taxi kwa barabara ya lami, ahadi hii nimeitimiza kikamilifu.
  37. Nawakaribisha nyote kujumuika nasi mchana wa leo Agosti 23, katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi kwenye viwanja vya Jangwani.
  38.   retweeted
    Usikose kujumuika pamoja nasi kesho kwenye uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya Jangwani.
  39. Ukaguzi ujenzi wa Daraja - Kigamboni Barabara: 6 Urefu: Mita 680 Upana: Mita 27.5 Muundo: Cable-Stayed
  40. Tumezindua kivuko cha MV Mafanikio kinachounganisha Semo-Msangamkuu, Mtwara. Mradi huu umegharimu TZS bilioni 3.3.
  41. Tatizo la barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi sasa ni historia, jana Agosti 7 imekamilika na tumeizindua rasmi.
  42. Watanzania wako makini na mustakabali wa nchi yao, wana imani kubwa na Chama Cha Mapinduzi, na watakipa ushindi ili kiendelee kuwatumikia.
  43. Ndugu zangu, sitawaangusha, na nitawatumikia ipasavyo. Rekodi yangu katika hilo iko wazi na dhahiri. Nitaeleza mengi kampeni zitakapoanza.
  44. 3. Mpango huu utatupa faida mbili; kwanza utapunguza msongamano Dar Es Salaam na pili utasaidia kuzuia uharibifu wa barabara zetu. - JPM
  45. 2. Badala ya magari ya mizigo kuingia Dar Es Salaam, utaratibu uwe kwamba yatachukua mizigo toka Ruvu itakapopelekwa kwa njia ya reli. - JPM
  46. 1. Kama Waziri wa Ujenzi ningependa tuboresha na kutumia reli kusafirisha mizigo toka Bandari ya Dar Es Salaam hadi eneo la Ruvu. - JPM
  47. Utumishi = Kujifunza + Kujitoa. Miaka 40 iliyopita, Machi 1975 nikiwa mwanafunzi, Kidato cha Kwanza Katoke Seminari.
  48. Ndugu zangu, mimi si mkali bali ninawachukia sana watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu wao; watumishi wa namna hiyo hawavumiliki. - JPM
  49. Watanzania wote wanahitaji maendeleo. Watanzania hawapendi kulalamika, wanahitaji kiongozi atayechapa kazi sawa sawa kutatua kero zao. - JPM
  50. Tumeungana pamoja, Chama Cha Mapinduzi ni kundi moja lenye nia moja ya kutumikia Watanzania kwa umoja na uimara wake. - JPM
  51. Nasema haya kutoka moyoni, nasema haya kwa dhati kabisa. Nawahakikishia nitakuwa nanyi, nitakuwa mtumishi wenu kweli kweli. - JPM
  52. Sasa ni wakati wa ndugu zangu watia nia wote 37, kuungana kupeperusha bendera ya Chama, kushinda kwa kishindo & kuwatumikia wananchi. - JPM
  53. Idadi ya kura za Wajumbe katika kunipitisha kuwa Mgombea Urais ni uthibitisho wazi kwamba CCM ni moja, na wana CCM ni wamoja. - JPM
  54. Nitumeni, nami nitawatumikia. Nakishukuru Chama Cha Mapinduzi, kwamba kimekubali kunituma kuomba ridhaa ya kuwatumikia Watanzania. - JPM
  55. Nimepewa heshima kubwa sana na dhahiri. Naahidi kuilipa heshima hii kwa kuinadi na kuitekeleza Ilani ya CCM katika kujenga Taifa letu. - JPM

2 comments:

Unknown said...

As Tanzanian i feel we are very blessed having such kind guy . He is a very uptodate and i like the way how open he is. He is extremely honest and hard working guy as well. I hope he will succeed to be our commander in chief we surely need such kind guy to be our leader no doubt he can make a very good presidency in our country. I believe we don't have such many kind leaders of his type in our country so is up to us tanzanians either we use him to fix our country and move forward or we lose him and staying with our miseries from the sluggish and corrupted leaders.

Anonymous said...

Miaka19 kidato channe?