ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 24, 2015

UCHAFU WA MAGANDA YA MIWA WAZIBA MTARO WA MAJI MACHAFU SOKO LA MIEMBENI MJINI DODOMA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtaro wa kupitishia maji machafu hasa wakati wa mvua unakaribia kuzibwa na maganda ya miwa yanayomwagwa na wafanyabiashara wa miwa waliopo soko la Miembeni mjini Dodoma.Picha na John Banda
 Baadhi ya watu wanaonekana wakikusanyia takataka za maganda ya miwa kwenye mtaro unakatisha katika soko la Miembeni mjini Dodoma hali ambayo ni hatari kwa mtaro huo kuziba na kusababisha maji ya mvua zinazokaria kuanza mjini humo kutwama.


Maji machafu ambayo yamekuwa yakitolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ya General yametuama kutokana na ubovu wa miundombinu uliopo katika mtaro unayatililisha maji hayo katika eneo la soko la Miembeni mjini humo.

1 comment:

Anonymous said...

Kwa jinsi hii Kipindupindu kisiwepo. Halafu tunajiuliza kimeingiaje?? Viongozi wa serikali ya mtaa wapo na wanaona. Hawawajibiki kuweka nguvu pamoja kufanya usafi?? Nani awafanyie? Wananchi waanze kwa pamoja. Watu wetu wanakufa kwa kitowajibika.!!.