Baadhi ya akina mama na watoto wao wakitafutia chochote katika Dampo ambalo si Rasmi lililopo pembezoni mwa Barabara ya 12 karibu na kituo cha Daladala ziendazo Nkuhungu Jamatini bila kujali maambukizi ya magonjwa, huku wahusika wakioneka kutokujali
wakati ugonjwa wa kipindupindu ukiwa unazidi kushika kasi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam huko mkoani dodoma nako inasadikika kwamba ugonjwa huo umekwisha gonga hodi huku wakazi wa maeneo mbalimbali wakionekana kusambasa hovyo uchafu na wengine kuwa katika sehemu hatarishi za kuweza kupata ugonjwa huo
katika barabara ya kumi na mbili (12) huko mkoani Dododma pembezoni kidogo mwa barabara kumeonekana baadhi ya wakazi wa mji huo wakiwa katika sehemu za kutupia taka na kuzihifadhi kwaajiri ya kuzichoma arimaarufu kama (Dampo) bila kuogopa tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu ,licha ya serikali kila siku kupiga kelele kuhusiana na usafi na utunzaji wa mazingira wa miji yetu hali imekuwa tofauti na mapokeo ya wananchi kwani wamekuwa wakikaidi na kuweka taka hizo sehemu zisizo stahili bila kujali afya zao
Tunza mazingira ili uepukane na magojwa ya mlipuko epuka uchafu ili uwe na afya bora
No comments:
Post a Comment