
Viongozi
wote wa CCM wa kata ya mkomazi na pamoja na wapiga kura 1,400 wa eneo hilo
wilayani Korogwe wamejiunga na CHADEMA huku baadhi yao wakiamua kugombea nafasi
mbali mbali za uongozi kwa tiketi ya chama hicho.
Wakizungumza
katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika kijiji cha mikocheni kilichopo kata
ya mkomazi wilayani Korogwe baadhi ya viongozi hao pamoja na wengine wa CCM
katika kata sita waliokatwa majina yao katika zoezi la kura za maoni kwa tiketi
ya CCM wamesema wameamua kujiunga na chadema pamoja na wapiga kura wao
ili kuongeza nguvu kupata wawakilishi wa wananchi katika baraza la madiwani la
halmashauri ya wilaya ya Korogwe.
Kwa upande
wake katibu wa CHADEMA jimbo la Korogwe Bwana.Salim Sempoli amemuomba
mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la Korogwe kuharakisha malalamiko
ya wapiga katika baadhi ya vituo ambapo sehemu kubwa ya majina ya wapiga kura
katika jimbo la Korogwe vijijini hayaonekani na hadi sasa hakuna utaratibu
uliofanywa kusaidia tatizo hilo kwa sababu linaweza kuleta viashiria vya
uvunjifu wa amani wakati wa zoezi la kupiga kura.
Kufuatia
hatua hiyo mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Emmanuel Kimea amewataka
wananchi kuwachagua viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya taifa,ubunge na
udiwani kwa sababu ndani9 ya chama kikoja changamoto zinazowakabili katika kata
ya mkomazi ikiwemo ya migogoro ya ardhi haiwezi kumalizika kama hawatafanya
mabadiliko.
CHANZO: ITV TANZANIA
1 comment:
Pure baseless propanda to counter NCCR MAGEUZI revolt and that is gonna help in reality.
Post a Comment