Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-IRINGA
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda nafasi ya Urais.
Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Magufulika staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga push up kama ionekanavyo pichani.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani Iringa.
Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
Vimbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda mapema .
wazee wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema katika Mji wa Ilula Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
1 comment:
Serikali yaamriwa kulipa meli, `samaki wa Magufuli`
Written by Ashakh (Kiongozi) // 27/09/2015 // Habari // Maoni 1
me » News
Serikali yaamriwa kulipa meli, `samaki wa Magufuli`
BY HELLEN MWANGO
26th August 2014
Email
Print
Dk. John Magufuli
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeamuru Serikali ya Tanzania kulipa meli ya uvuvi pamoja na samaki waliokamatwa miaka mitano iliyopita mali ya raia wa China, vyote vikiwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 3.2.
Mahakama hiyo imetoa amri hiyo baada ya kuwaachia washtakiwa wawili raia wa China, Hsu Tai na Zhao Hanquing, waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuvua samaki katika Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania bila kibali, maarufu ‘Samaki wa Magufuli’.
Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Wakili wa Utetezi, Kapteni Ibrahim Bendera, alisema meli iliyokamatwa na wateja wake ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 2.5 na samaki waliokutwa nao walikuwa na thamani ya Dola za Marekani 720,000.
“Bado tunasubiri maelekezo ya wamiliki wa hiyo meli kuhusu hatua za kisheria zinazostahili ili wapate fedha hizo” alisema Kapteni Bendera kwa njia ya simu.
Agosti 22, mwaka huu, Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Isaya Arufani, alisoma uamuzi wa kuwaachia huru Wachina hao, pamoja na mambo mengine, aliamuru serikali kulipa mali hizo pamoja na hati zao za kusafiria.
Kesi hiyo awali ilikuwa ikiwakabili watu 38 kutoka mataifa tofauti ya Bara la Asia ya China, Ufilipino, Vietnam na wawili raia wa Kenya.
Walikamatwa Machi 8, mwaka 2009 wakivua na walikutwa na tani 293 za samaki, wakati huo, Dk, John Magufuli akiwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Kati ya washtakiwa hao, mmoja alifariki dunia, wengine 35 waliachiwa huru na wawili kutiwa hatiani.
Hakimu Arufani aliwaachia huru washtakiwa hao wiki iliyopita ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashitaka hayo.
SOURCE: NIPASHE
Post a Comment